20. Maneno ya ´Atwaa´ bin Yasaar kuhusu mikono ya Allaah

19- Imesihi kutoka kwa Khaarijah bin Musw´ab: Zayd bin Aslam ametuhadithia, kutoka kwa ´Atwaa´ bin Yasaar ambaye amesema:

“Malaika walisema: “Ee Mola! Umewaumba watu na kuwafanya ni wenye kula, wenye kunywa na kustarehe na wanawake. Hukutujaalia sisi chochote katika hayo. Ikiwa Umewajaalia dunia basi Tujaalie na sisi Aakhirah.” Ndipo Allaah (´Azza wa Jall) akasema: “Sintojaalia kizazi cha Niliyemuumba kwa mkono Wangu kiwe kama kile nilichoumba kwa kusema “Kuwa!” na kikawa”.

Namna hii ndivo alivopokea Khaarijah.

20- Ameipokea pia ´Abdullaah bin Swaalih, kutoka kwa al-Layth, kutoka kwa Hishaam bin Sa´d, kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa ´Atwaa’ bin Yasaar, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Cheni ya wapokezi ni Swahiyh na imethibiti na imepokelewa na ´Uthmaan bin Sa´iyd ad-Daarimiy kutoka kwa ´Abdullaah bin Swaalih.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 22
  • Imechapishwa: 25/06/2019