Swali 20: Unasemaje kwa mwenye kusema:

“Magomvi yetu na mayahudi sio ya kidini. Kwa sababu Qur-aan inatuamrisha kuwaonyesha mapenzi na urafiki.”[1]

Jibu: Maneno haya yana mkanganyiko na upotofu. Mayahudi ni makafiri. Allaah (Ta´ala) amesema kuwa ni makafiri na amewalaani, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwa ni makafiri na amewalaani. Allaah (Ta´ala) amesema:

لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ

“Wamelaaniwa wale waliokufuru ambao ni wana wa israaiyl kwa ulimi wa Daawuwd na ‘Iysaa mwana wa Maryam – hivyo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakipindukia mipaka.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Laana ya Allaah iwe juu ya mayahudi na manaswara.”[3]

Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ أُولَـٰئِكَ هُمْ شَرُّ الْبَرِيَّةِ

“Hakika wale waliokufuru ambao ni Ahl-ul-Kitaab na washirikina watakuwa katika Moto wa Jahannam – ni wenye kudumu humo; hao ndio waovu wa viumbe.”[4]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ

“Enyi mlioamini! Msiwafanye mayahudi na manaswara marafiki – wao kwa wao ni marafiki.”[5]

Magomvi yetu na mayahudi ni ya kidini. Haijuzu kwetu kuwa na urafiki nao wala kuwapenda. Kwa sababu Qur-aan imetukataza hilo, kama ilivyo dhahiri katika Aayah zilizotajwa.

[1] Haya yalisemwa na Hasan al-Bannaa, muasisi wa al-Ikhwaan al-Muslimuun. Rerejea katika kitabu “al-Ikhwaan al-Muslimuun Ahdaath swan´at at-Taariykh” (1/409) cha Mahmuud ´Abdul-Haliym.

Mfano wa maneno kama haya ya khatari yamesemwa na Muhammad al-Mas´ariy Khaarijiy. Pamoja na kwamba watu hawa wawili wana mifumo yenye kutofautiana lakini maneno yao ni yenye kufanana. Kitu kinachowakutanisha tu ni mfumo wa kiharakati. Mtu huyu ambaye amebadili kilicho duni kwa kilicho bora zaidi wakati alipohama kutoka mji wa misikiti miwili Mitakatifu na mji wa Tawhiyd na akaenda kuishi katika mji wa kikafiri na kuridhia kuhukumiwa na kufuru. Alisema:

“Kwa sasa Saudi Arabia haiwaruhusu wakristo na mayahudi kuonyesha waziwazi nembo zao za ´ibaadah. Mambo yatabadilika pale ambapo kamati (ile inayodaiwa kuwa ni kamati ya kutetea haki za binaadamu) itapopata nguvu na kuwapa idadi ndogo ya watu haki zao. Wapata kuoana kutokana na nembo zao na kufanya mengine yote ndani ya makanisa yao. Watapata kufanya mambo mengine yote kikamilifu. Haijalishi kitu ni mamoja watakuwa mayahudi, wakristo au wahindu.” (Gazeti “ash-Sharq al-Awsatw” (06/2670), Jumapili 08 Ramadhaan 1416)

Amesema vilevile:

“Hakika kujenga makanisa inajuzu kwa mujibu wa Shari´ah ya Kiislamu.” (Chanzo hichohicho kilichoko juu)

“Mwendesha kipindi kwenye redio ya kingereza alisema:

“Mpinzani wa kisaudi Muhammad al-Mas´ariy anayeishi London na ambaye anajiita kuwa ni “Jihaadiy” amesema kwamba atapanga mkutano wa wanahabari kabla ya kuisha kwa mwezi huu pamoja na wapinzani wa Shiy´ah ili kutangaza chombo kimoja pamoja na wao.”

Kisha al-Mas´ariy akasema mwenyewe:

“Kutakuwepo utaratibu na pengine hata kutakuwepo chombo kipana. Tunafanya kazi na kupambana kwa ajili ya hilo. Ni harakati za Kiislamu ni mamoja iwe zinahusiana na harakati za ki-Sunniy au za ki-Shiy´ah. Ni harakati za Kiislamu ambazo kuna maafikiano juu yake na Uislamu pasi na ubishi wowote. Utawafanya waislamu wote kuwa na umoja; Sunnah na Shiy´ah. Kutokana na hilo tutaweza kuzihifadhi haki za waislamu na za wananchi. Tunazitambua haki zao wananchi wote; mayahudi, manaswara, waabudia moto na wengineo katika miji ya Kiislamu. Kwa hivyo harakati zetu ni za kisiasa zilizojengwa juu ya misingi ya Kiislamu na sio makundi wala madhehebu.” (1417/06/29)

Hivi kweli kuna upofu ulio mkubwa na ujasiri dhidi ya Uislamu kushinda huu? Ni upi msimamo wa al-Mas´ariy kuhusiana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Waondosheni washirikina katika kisiwa cha Kiarabu.” (al-Bukhaariy (2888, 2997 na 4168))

”Dini mbili hazikusanyiki katika kisiwa cha Kiarabu”? (Maalik (1862) na al-Bayhaqiy (09/208))?

Je, inamstahikia kweli mtu ambaye ni mjinga juu ya Hadiyth kama hizi zilizo wazi kuwa mwelekezaji au kiongozi ikiwa kama sio kiongozi mwenye kuongoza katika upotevu na matamanio? Ni kana kwamba ni mwenye kujisalimisha kwenye maneno ya mshairi:

Wapake mafuta muda wa kuwa uko nyumbani kwao

waridhishe muda wa kuwa uko nchini mwao

Muftiy mkubwa, Imaam na Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

“Vipeperushi hivi vinavyotoka kwa al-Faqiyh, al-Mas´ariy au mtu mwengine katika walinganiaji wa batili na walinganiaji wa shari, ni lazima kuviharibu, kuvichana na kuvipuuza. Ni lazima kwa yule anayeweza awanasihi, kuwaongoza katika haki na kuwatahadharisha na batili. Haijuzu kwa yeyote kushirikiana nao katika shari hii. Ni lazima wanasihiwe na warejee katika haki. Ni wajibu kwao kuachana na batili hii.

Nasaha yangu kwa al-Mas´ariy, al-Faqiyh, Ibn Laadin na wengine wote wanaopita katika mfumo wao, wajiweke mbali na njia hii mbaya na badala yake wamche Allaah kwa yale waliyofanya hapo kabla.” (Majmuu´-ul-Fataawaa (09/100))

[2] 05:78

[3] al-Bukhaariy (425) na Muslim (531).

[4] 98:06

[5] 05:51

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 65-66
  • Imechapishwa: 31/05/2023
  • mkusanyaji: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy