20. Kutenga wakati wa kufanya marejeleo

Kuna kitu nataka kukizindua. Mwanafunzi anatakiwa kutenga wakati wa kufanya marejeleo kwa yale aliyoyasoma. Ama mwanafunzi kujifunza kitu kisha akakisahau baada ya hapo na wala asikirudilii, hakika hili halimnufaishi kitu mwanafunzi.

Mwanafunzi anatakiwa kujipangia wakati wa kufanya marejeleo. Bora zaidi akifanya marejeleo na rafiki mwingine. Kwa mfano anaweza kutenga wakati wa kufanya marejeleo ya kila siku kwa njia ya kwamba kila siku baada ya kumaliza kusoma darsa fulani, anafanya marejeleo na rafiki yake kile alichokisoma na kila mmoja akaorodhesha vipengele vya faida alivyojifunza. Kisha afanye marejeleo ya wiki. Kwa mfano atenge wakati siku ya ijumaa ambapo anarudilia yale aliyofaidika katika wiki hii. Kisha afanye marejeleo ya mwezi. Kwa mfano atenge siku moja katika mwezi ambapo anarudilia yale aliyojifunza. Aendelee namna hii. Hivi ndivyo walivyokuwa wakifanya Salaf.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Ilm wa Wasaaailuh wa Thimaaruh
  • Imechapishwa: 22/10/2016