20. Hali ya leo inajuzisha kuwepo kwa watawala wengi

Vile ninavyoonelea mimi ni kwamba hali ilivyo leo hii ni kwamba imekuwa ni jambo la kidharurah kwa sababu ya mambo yafuatayo:

1- Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Wana wa israaiyl walikuwa wakiongozwa na Mitume. Kila anapofariki Mtume basi anakuja nafasi yake Mtume mwingine. Pamoja na kwamba hakuna Mtume mwingine baada yangu lakini hata hivyo watakuwepo makhaliyfah wengi.” Wakasema: “Unatuamrisha nini?” Akasema: “Toeni kiapo cha utiifu kimoja baada ya kingine na wapeni haki zao. Allaah atawauliza juu ya kile alichowatawalisha.”[1]

Hadiyth hii inaashiria kwamba inafaa kuwepo kwa watawala wengi ikiwa kila mmoja anasimamia nchi yake. Hata hivyo haitofaa kuwepo kwa watawala wengi katika nchi moja. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Wakipewa kiapo cha utiifu makhaliyfah wawili basi muueni yule wa mwisho wao.”[2]

“Atakayekujieni ilihali mmekusanyika juu ya mwanaume mmoja na anataka kutawanyisha umoja wenu, basi kateni shingo yake yoyote awaye.”[3]

Hilo limeashiria Hadiyth iliotanuglia:

“Toeni kiapo cha utiifu kimoja baada ya kingine… “

2- ´Aliy bin Abiy Twaalib na Mu´aawiyah (Rahidhiya Allaahu ´anhumaa) wote wawili kila mmoja alisimamia nchi yake. Humo walisimamisha na kutekeleza adhabu na hukumu za Allaah. Kipindi hicho Maswahabah walikuwa wamejaa na hakuna hata mmoja aliyeonelea mmoja katika makhaliyfah hao wawili kwamba serikali yake ni batili. Kadhalika kuhusu tamko la uhuru wa Andalusia mwishoni mwa wakati wa Taabi´uun.

3- Kutokana na kupanuka na kuenea kwa Uislamu ilikuwa ni jambo la kidharurah kuwepo kwa watawala wengi. Kwa sababu mtu mmoja hawezi kusimamia nchi zote hizi pasi na kuwa na magavana wa kujitegemea. Hiyo ni dalili inayofahamisha juu kufaa kuwepo kwa watawala wengi.

[1] al-Bukhaariy (3455) na Muslim (1842).

[2] Muslim (1853).

[3] Muslim (1852).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 42-43
  • Imechapishwa: 03/12/2018