20. Hadiyth ”Tumesoma katika Kitabu cha Allaah (Ta´ala) ya kwamba siku ya ijumaa kuna saa… “


702- ´Abdullaah bin Salaam ameeleza:

”Nilisema na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekaa: ”Tumesoma katika Kitabu cha Allaah (Ta´ala) ya kwamba siku ya ijumaa kuna saa ambayo hakutani nayo mja muumini ambapo amesimama anaswali na kumuomba Allaah kitu isipokuwa Allaah anamkhidhia haja yake.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaashiria kwangu kama vile anasema: “Au baadhi ya saa.” Nikasema: “Umesema kweli; au baadhi ya saa. Ni saa gani hiyo?” Akajibu: “Ni saa za mwisho za mchana.” Nikasema: “Kwa hiyo sio saa ya swalah.” Akasema: “Ndio. Mja akishaswali kisha akaketi na kusiwepo na kitu kilichomkalisha isipokuwa swalah basi anazingatiwa bado yuko katika swalah.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah na mlolongo wa wapokezi wake uko kwa mujibu wa masharti ya Swahiyh.

[1] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/439)
  • Imechapishwa: 13/01/2018