20- Yahyaa bin ´Ammaar al-Imaam ametuhadithia: Ibn Swabaah ametuhadithia: Ishaaq ametuhadithia… ح Ibn-ul-Fadhwl az-Zaahid ametuhadithia: Muhammad bin al-Fadwhl bin Muhammad bin Ishaaq bin Khuzaymah ametuhadithia: Babu yangu ametuhadithia: al-Muqriy ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia: Harmalah bin ´Imraan ametuhadithia: Abuu Yuunus Sulaym bin Jubayr amenihadithia: Nilimsikia Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) akisoma Aayah hii:

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ النَّاسِ أَن تَحْكُمُوا بِالْعَدْلِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ سَمِيعًا بَصِيرًا

“Hakika Allaah anawaamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe na mtakapohukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Ni uzuri wa anayokuwaidhini nayo Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (04:58)

Halafu akaweka kidole chake cha gumba kwenye sikio lake na kidole chake cha shahaadah kwenye jicho lake na kusema: “Hivi ndivyo nilivyomsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiisoma na akaweka vidole vyake juu yavyo.”[1]

Matamshi ni ya Ibn Khuzaymah.

[1] Abuu Daawuud (4728), Ibn Khuzaymah katika ”Kitaab-ut-Tawhiyd”, uk. 42-43, Ibn Hibbaan (265), al-Haakim (1/24) na al-Laalakaa’iy (688).

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 46
  • Imechapishwa: 25/01/2017