2- Kufa kwa kutokwa na jasho kwenye paji la uso. Hilo ni kutokana Hadiyth ya Buraydah  bin al-Khaswiyb (Radhiya Allaahu ´anh):

“Alikuwa Khuraasaan ambapo akamtembelea ndugu yake mmoja aliyekuwa mgonjwa. Alikuwa katika hali ya kutaka roho. Tahamaki jasho likaanza kumtoka kwenye paji la uso. Akasema: “Allaahu ni mkubwa! Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Muumini anakufa kwa kutokwa la jasho kwenye paji la uso.”

Ameipokea Ahmad (05/357, 360) na mtiririko ni wake, an-Nasaa´iy (01/259), at-Tirmidhiy (02/128) ambaye ameifanya kuwa ni nzuri, Ibn Maajah (01/443-444), Ibn Hibbaan (730), al-Haakim (01/761), at-Twayaalisiy (808). al-Haakim amesema: “Swahiyh juu ya sharti za Muslim” na adh-Dhahabiy ameafikiana naye. Kuna jambo la kujadili, lakini hapa si pahali pa kulitaja khaswa kwa kuzingatia kwamba moja katika cheni za wapokezi za an-Nasaa´iy ni Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy. Hadiyth hiyo ina ushahidi kutoka katika Hadiyth ya ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh). Ameipokea vilevile at-Twabaraaniy katika “al-Awsatw” na “al-Kabiyr” na wapokezi wake ni wapokezi Swahiyh, kama ilivyo katika “al-Majma´” (02/325).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 49
  • Imechapishwa: 08/01/2020