اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ

“Tuongoze njia iliyonyooka.”[1]

“Njia ya kuwatambua maimamu. Tafsiri hii imenasibishwa kwa Abu ´Abdillaah [Ja´far as-Swaadiq] ambaye amesema:

“Njia iliyonyooka ni kiongozi wa waumini. Dalili ya hilo ni Kauli Yake:

وَإِنَّهُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ

“Na hakika hii iko katika Mama wa Kitabu Kwetu, bila shaka ni yenye shani ya juu (علي) [kimetukuka], yenye hikmah.”[2]

Ni kiongozi wa waumini katika mama wa kitabu.”[3]

Huu ni upotoshaji wa fedheha kwa Kitabu cha Allaah unaoenda kinyume na siyaki ya maelezo ya wazi. Allaah amebainisha makusudio ya njia iliyonyooka na kusema:

اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ

“Tuongoze njia iliyonyooka – Njia ya wale Uliowaneemesha.”[4]

Watu walioneemeshwa na Allaah ni wale ambao Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) amewataja katika Kitabu Chake kilicho wazi:

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا

“Na atakayemtii Allaah na Mtume, basi hao watakuwa pamoja na wale ambao Allaah Amewaneemesha miongoni mwa Manabii na wakweli na mashahidi na [waja] wema – na uzuri ulioje hao kuwa ni rafiki [zake].”[5]

Inawahusu Manabii wote, Mitume, wakweli na waja wema waliomfuata Mtume na kutoka katika Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Tazama jinsi Raafidhwah wanavofasiri Kitabu cha Allaah kwa matamanio yao! Lau muislamu atafuata ujumbe wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika ´Aqiydah na matendo pasina kumjua ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu), hilo halitomdhuru kitu. Hakuna yeyote atayeulizwa siku ya Qiyaamah wala ndani ya kaburi juu ya ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu). Allaah atawauliza watu kuhusu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ujumbe wake.

Amesema:

“Dalili ya hilo ni Kauli Yake:

وَإِنَّهُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ

“Na hakika hii iko katika Mama wa Kitabu Kwetu, bila shaka ni yenye shani ya juu (علي) [kimetukuka], yenye hikmah.”[6]

Ni kiongozi wa waumini katika mama wa kitabu.”

Huu ni upotoshaji mkubwa na mchezo wa Kitabu cha Allaah. Maelezo haya yanaelekezwa katika Qur-aan. Allaah (Ta´ala) Amesema:

حم وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ إِنَّا جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ وَإِنَّهُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ

Haa Miym. Kwa Kitabu kinachobainisha. Hakika Sisi Tumeifanya Qur-aan [kwa] Kiarabu ili mpate kutia akilini. Na hakika hii [Qur-aan] iko katika Mama wa Kitabu Kwetu, bila shaka ni yenye shani ya juu [kimetukuka], yenye hikmah.”[7]

Kusema kuwa Aayah zinamuhusu ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anhu) ni upotoshaji na uongo juu ya Allaah na Kitabu Chake.

[1] 01:06

[2] 43:04

[3] Tafsiyr al-Qummiy (01/28-29).

[4] 01:06-07

[5] 04:69

[6] 43:04

[7] 43:01-04

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 52-53
  • Imechapishwa: 19/03/2017