2- Lililo la wajibu kwa kila muislamu kumuhifadhi Allaah kwa njia ya mtu kuchunga yale aliyoamrisha na kujiepusha na makatazo Yake. Kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia Ibn ´Abbaas:

”Muhifadhi Allaah Naye atakuhifadhi. Muhifadhi Allaah utamkuta mbele Yako.”

Kuchunga maamrisho ya Allaah hali ya mtu kutekeleza maamrisho na kuyaacha makatazo ni sababu ya kulindwa kwa mja, kusalimika kwake na Allaah kumuhifadhi duniani na Aakhirah. Akifikwa na msiba au akateremkiwa na madhara basi anakuwa ni mwenye kupandishwa daraja mbele ya Allaah. Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu ya haya:

”Ajabu iliyoje juu ya hali ya muumini. Kwani hakika hali zake zote huwa ni kheri. Hayo hayawi kwa yeyote isipokuwa kwa muumini pekee. Anapofikwa na jambo zuri, basi hushukuru na ikawa ni kheri kwake. Na anapofikwa na jambo la madhara, basi husubiri na ikawa ni kheri kwake.”[1]

[1] Muslim (2999).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://ar.islamway.net/article/80439/%D9%81%D9%8A%D8%B1%D9%88%D8%B3-%D9%83%D9%88%D8%B1%D9%88%D9%86%D8%A7-%D8%A7%D9%84%D8%AC%D8%AF%D9%8A%D8%AF-%D9%81%D9%8A%D8%B1%D9%88%D8%B3-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%8A%D9%86
  • Imechapishwa: 09/03/2020