2. Utekaji nyara, mauaji na milipuko ni mifano ya ugaidi


Ni jambo lisilokuwa na shaka kabisa kwamba ugaidi hii leo umekuwa ni katika mambo makubwa katika mazingira ya kimataifa na imekuwa ni jambo lenye kuzishughulisha jamii zote pasina kujali dini, mielekeo na nidhamu. Kama ilivyo miji mingine yote miji ya Kiislamu vilevile imechukua sehemu ya ugaidi na tofauti zake.

Nini maana ya ugaidi? Kipi kilicho nyuma yake? Ni madhara yepi yanayozalikana kwa matendo haya maovu ya magaidi madhalimu?

Ugaidi unatendeka kwa sura mbalimbali lakini mjumuiko wake ni kuwashtua na kuwatia khofu watu wenye amani. Baada ya hapo ugaidi ukapita khofu na woga na kuanza kuzimwaga damu za watu wasiokuwa na hatia, kuziharibu na kuzipora mali takatifu, kuzivunja heshima zilizohifadhiwa na kutawanyisha mkusanyiko. Matokeo yake kwenye neema kunaingizwa badala yake mitihani na majanga. Natija yake ufisadi unaanza kuenea juu ya ardhi, ile harufu yake mbaya inawazunguka viumbe. Kwa msemo mwingine:

1- Watu walioko kwenye vyombo vya usafiri na wenye kutembea kwa miguu mabarabarani kutekwa nyara, kuuawa kwa viongozi na milipuko kwenye vifaa vya kimataifa na vya kitaifa kwa lengo la kuharibu si jengine isipokuwa ni mfano katika mifano ya ugaidi iliyooza na yenye fitina.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Irhaab, uk. 11
  • Imechapishwa: 31/03/2017