Ndugu! Allaah (Ta´ala) amesema:

مَّا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِن شَيْءٍ

”Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote.”[1]

Kuna ambao wamefasiri kuwa Kitabu kunamaanishwa Qur-aan. Si kweli. Kitabu kunalengwa Ubao uliohifadhiwa. Kuhusu Qur-aan Allaah (Ta´ala) ameisifu kiwaziwazi kabisa kuliko njia yenye kukanusha pale aliposema:

وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَانًا لِّكُلِّ شَيْءٍ

“Na Tumekuteremshia Kitabu hiki kinachobainisha kila kitu.”[2]

Aayah hii iko wazi na bainifu zaidi kuliko:

مَّا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِن شَيْءٍ

”Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote.”

Huenda mtu akauliza ni wapi Qur-aan imetaja swalah tano na idadi ya Rak´ah zake. Ni vipi itawezekana kwa sisi kutoweza kupata katika Qur-aan idadi ya Rak´ah zote ilihali Allaah anasema:

وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَانًا لِّكُلِّ شَيْءٍ

“Na Tumekuteremshia Kitabu hiki kinachobainisha kila kitu”?

Jibu ya hilo ni kwamba Allaah (Ta´ala) ametuwajibishia katika Qur-aan kurejea kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ ۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا

“Atakayemtii Mtume basi kwa hakika amemtii Allaah; na atakayekengeuka, basi hatukukutuma kuwa mlinzi juu yao.”[3]

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ

“Na lolote lile analokupeni Mtume basi lichukueni, na lolote lile analokukatazeni, basi acheni. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu.”[4]

Qur-aan imejulisha yale yaliyobainishwa na Sunnah. Kwa sababu Sunnah ni moja katika aina za Wahy ambao Allaah amemteremshia na kumfunza Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأَنزَلَ اللَّـهُ عَلَيْكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَعَلَّمَكَ مَا لَمْ تَكُن تَعْلَمُ ۚوَكَانَ فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكَ عَظِيمًا

“Na Allaah amekuteremshia Kitabu na Hekima na akakufunza yale ambayo hukuwa unayajua. Na fadhilah za Allaah juu yako ni kuu.”[5]

Kutokana na hili kila kilichoko katika Sunnah basi kipo pia katika Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall).

[1] 06:38

[2] 04:80

[3] 04:80

[4] 59:07

[5] 04:113

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ibdaa´ fiy Kamaal-ish-Shar´ wa Khatwar-il-Ibtidaa´, uk. 3-4
  • Imechapishwa: 23/10/2016