Hakika yeye ndiye kiongozi wa wanaadamu Abul-Qaasim Muhammad, Ahmad, al-Maahiy mwenye kutokomeza kufuru, al-Haashir mwenye kuwakusanya watu, al-Aaqib ambaye hakuna baada yake Nabii, al-Muqaffiy, Mtume wa rahmah, Mtume wa tawbah na Mtume wa kichinjwa. Alikuwa ni mtoto wa ´Abdullaah ambaye alikuwa ni ndugu wa kina al-Haarithiy, az-Zubayr, Hamzah, al-´Abbaas (Abul-Fadhwl), Abu Twaalib ambaye alikuwa akiitwa Abdu Manaaf, Abu Lahab ambaye alikuwa akiitwa ´Abdul-´Uzzaa, ´Abdul-Ka´bah ambaye pia alikuwa akiitwa al-Muqawwim na imesemekana kuwa ni watu wawili tofauti, Hujl ambaye pia alikuwa akiitwa al-Mughiyrah na al-Ghaydaaq ambaye aliitwa hivyo kwa sababu ya wingi wa kutoa kwake lakini ambaye alikuwa akiitwa Nawfal. Kauli nyingine ni kwamba alikuwa akiitwa Hujl na Dhwaraar.

Swafiyyah, ´Aatikah, Awraa´, Umaymah, Barrah na Umm Haakim (ambaye alikuwa akiitwa “mweupe”). Wote hawa walikuwa ni watoto wa ´Abdul-Muttwalib. Jina lake alikuwa akiitwa Shaybat-ul-Hamd kutokana na kauli sahihi. Alikuwa ni mtoto wa Hishaam aliyekuwa anaitwa ´Amr ambaye alikuwa ni ndugu wa al-Muttwalib. Kizazi cha Mtume kilikuwa kinahusiana na hao watu wawili. Halafu ´Abdu Shams na Nawfal watoto wao walikuwa ni wa ´Abdu Manaaf ambaye alikuwa ni ndugu wa ´Abdul-´Uzzaa, ´Abdud-Daar na ´Abd ambao walikuwa ni watoto wa Quswayy aliyekuwa akiitwa Zayd. Zayd huyu alikuwa ni ndugu wa Zuhrah ambaye alikuwa ni mtoto wa Kullaab ambaye alikuwa ni ndugu wa ´Aamir, Saamah, Khuzaymah, Sa´d, al-Haarith na ´Awf ambao walikuwa ni watoto wa Lu´ayy ambaye alikuwa ni ndugu wa Taym-ud-Adram. Wawili hao walikuwa ni watoto wa Ghaalib ambaye alikuwa ni ndugu wa al-Haarith na Muhaarib ambao walikuwa ni watoto wa Fihr. Fihr huyu alikuwa ni ndugu wa al-Haarith ambao walikuwa ni watoto wa Maalik ambaye alikuwa ni ndugu wa as-Salt na Yakhlad ambao walikuwa ni watoto wa an-Nadhr ambaye alikuwa ni ndugu wa Maalik, Malkaan, ´Abdu Manaaf na wengine ambao walikuwa ni watoto wa Kinaanah ambaye alikuwa ni ndugu wa Asad, Asdah na al-Hawn ambao walikuwa ni watoto wa Khuzaymah ambaye alikuwa ni ndugu wa Hudhayl ambaye alikuwa ni mtoto wa Madrakah aliyekuwa akiitwa ´Amr aliyekuwa ni ndugu wa Twabikhah aliyekuwa akiitwa ´Amr na Qama´ah ambao walikuwa ni watoto wa Ilyaas aliyekuwa ndugu wa an-Naas aliyekuwa akiitwa ´Aylaan baba wa Qays wote. Wote hawa wawili walikuwa ni watoto wa Mudhwar ambaye alikuwa ni ndugu wa Rabiy´ah ambao wanatokamana na kizazi za Ismaa´iyl na ndugu wa Anmaar na Iyaad. Wane hao walikuwa ni watoto wa Nazaar ambaye alikuwa ni ndugu wa Qadhwaa´ah kutokana na kauli wanahistoria wengi. Wawili hao walikuwa ni watoto wa Ma´ad ambaye alikuwa ni mtoto wa ´Adnaan. Makabila yote ya kiarabu yanajinasibisha na watoto wa ´Adnaan niliyowataja.

Haafidhw Abu ´Amr an-Namaariy (Rahimahu Allaah) amebainisha vya kutosha katika kitabu “al-Inbaah bi Ma´rifati Qabaa´il-ir-Ruwaah”:

“Quraysh kutokana na kauli ya wanahistoria wengi ni wale wanaojinasibisha kwa Fihr bin Maalik bin an-Nadhr bin Kinaanah.”

Mshairi anasema:

Ninaapa kuwa Quswayy alikuwa akiitwa Mkusanyaji

kupitia kwake Allaah ameyakusanya makabila yote kutoka Firh

Maoni mengine yanasema kuwa Quraysh inaanza kutoka kwa an-Nadhr bin Kinaanah. Wanachuoni na wahakiki wengi wana kauli hii. Ushahidi wa hilo ni ile Hadiyth iliyotajwa na Abu ´Umar bin ´Abdil-Barr (Rahimahu Allaah) kupitia kwa al-Ash´ath bin Qays (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesema:

“Nilikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nikiwa na jopo kutoka Kindah. Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Je, wewe si katika sisi?” Akasema: “Hapana. Sisi ni kizazi cha an-Nadhr bin Kinaanah. Hatuwatuhumu mama zetu kwa machafu na wala hatuwakanushi baba zetu.”[1]

Ibn Maajah amepokea katika “as-Sunan” mlolongo wa wapokezi ulio mzuri. Humo al-Ash´ath amesema:

“Hatonijia mtu mwenye kumkataa mtu kutoka katika Quraysh kutoka kwa an-Nadhr bin Kinaanah isipokuwa nitamtandika.”

Maoni mengine yanasema kuwa Quraysh inaanza kwa Ilyaas bin Mudhar bin Nazaar. Wengine wanasema kuwa inaanza kwa baba yake Mudhar. Kauli mbili hizo ni za baadhi ya Shaafi´iyyah, ambazo Abul-Qaasim ´Abdul-Kariym ar-Rifaai´iy amezitaja katika ufafanuzi wake. Licha ya kwamba kauli mbili hizo ni geni sana.

Kuhusiana na makabila ya Yemen kama Humayr, Hadhwramawt na Saba´, ni kweli kwamba ni zenye kutokamana na Qahtwaan na si ´Adnaan.

Kuna maoni tatu juu ya Qadhwaa´ah. Moja ni yenye kusema wanatokamana na ´Adnaan, nyingine inasema ni wenye kutokamana na Qahtwaan na ya tatu ni yenye kusema kuwa ni kabila la tatu kando na si kutokamana na hawa wala hawa. Ni kauli geni iliyotajwa na Abu ´Umar na wengine.

[1] Ahmad (5/211). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaami´” (6753).

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 11-12
  • Imechapishwa: 18/03/2017