2. Mfano wa pili kuonyesha kuwa Raafidhwah ni Baatwiniyyah


2- al-´Ayyaashiy (02/16) amesema:

“Muhammad bin Mansuur ameeleza kuwa alimuuliza mja mwema kuhusiana na Kauli Yake (Ta´ala):

قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ

“Sema: “Hakika Mola wangu Ameharamisha matendo machafu, yaliyodhihirika na yaliyo ya siri…” (07:33)

Akasema: “Qur-aan ina udhahiri na undani wake. Kila kile ambacho Qur-aan imeharamisha ni kwa udhahiri na kwa undani ikiwa ni pamoja na viongozi madhalimu. Na kila kile ambacho Qur-aan imehalalisha ni kwa udhahiri na kwa undani ikiwa ni pamoja na viongozi wa haki.”

Mhakiki ameelekeza katika “al-Bihaar” na “al-Burhaan”.

Hatumjui ni nani huyu mja mwema. Lakini ni dhahiri kwamba ni mmoja katika viongozi wakubwa wa Baatwiniyyah. Viongozi madhalimu anayemkusudia huyu Baatwiniy kwanza ni Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhum). Viongozi wa haki anakusudia Ahl-ul-Bayt ambao Raafidhwah/Baatwiniyyah wamejifichika nyuma yao ili wapate kuubomoa Uislamu na kuipotosha Qur-aan kwa kutumia jina lao.

Haki ni kwamba makusudio ya matendo machafu ni maasi yanayofanywa hadharani na yaliyo ya siri ni yale yanayofanyika kwa kujificha. Matendo machafu ni yale yaliyopindukia kwa ubaya kama mfano wa uzinzi na kujamiiana na Mahaarim.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 29-30
  • Imechapishwa: 18/03/2017