Maendeleo ya pili:

Maendeleo ya pili yalionekana kwenye gazeti “Aakhiru Saa´ah” lililotoka siku ya ijumaa tarehe 05 aprili 1946. Hapo ndipo kiongozi wa jumla wa al-Ikhwaan al-Muslimuun Hasan al-Bannaa alipopata pendekezo kutoka kwa wakristo wa raia wa Misri [copts] kuita al-Ikhwaan al-Muslimuun “al-Ikhwaan al-Miswriyyuun” ili wakristo wengi na wao waweze kujiunga nao. Pendekezo hili bila ya shaka ni matunda ya maendeleo ya kwanza.

Ni dini ipi iliyobaki kwa al-Ikhwaan al-Muslimuun ikiwa watu wote pasina kujali dini ni ndugu zao? Wanapopata pingamizi kwa Kauli ya Allaah (Ta´ala):

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ

“Hakika si venginevyo waumini ni ndugu.”[1]

wanasema kuwa waumini ni waumini kwa fikira zao.

Kuhusiana na maandiko ya wazi yaliyothibiti ambayo yanatahadharisha kuwafanya makafiri kuwa ni marafiki ikiwa ni pamoja na Kauli ya Allaah (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ

“Enyi mlioamini! Msiwachukuwe mayahudi na manaswara [kuwa ndio] marafiki walinzi – wao kwa wao ni marafiki walinzi – na yeyote atakayewafanya marafiki, basi hakika yeye ni miongoni mwao.”[2]

pengine kiongozi wa jumla (Hasan al-Bannaa) anaweza kutafuta tafsiri atayoitumia inayoendana na yeye kwa vile ni mtu mkubwa wa hila na mwenye vishindo.

[1] 49:10

[2] 05:51

  • Mhusika: Shaykh Ahmad Shaakir, Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Afiyfiy, Shaykh ´Abdur-Rahmaan al-Wakiyl, Shaykh Muhammad Khaliyl al-Harraas, Shaykh Muhammad Haamid al-Faqiy na wengineo.
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Lamahaat ´an Da´wat-il-Ikhwaan al-Muslimiyn, uk. 9-10 Gazeti al-Hadiy an-Nabawiy (1365/6)
  • mkusanyaji: Muhammad bin ´Iwadhw bin ´Abdil-Ghaniy