2. Kupangusa kumefutwa?


Swali 02: Nini maana ya maneno ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakupangusa baada ya kuteremshwa Suurah ”al-Maaidah” na maneno ya ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) ”Kitabu kimetangulia jambo la kufuta”?

Jibu: Sijui kama hayo yamesihi kutoka kwa wawili hao (Radhiya Allaahu ´anhumaa). ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) ni mmoja katika wale waliopokea Hadiyth zinazozungumzia kufuta kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ameisimulia baada ya kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akabainisha kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameweka muda wa upangusaji. Ni dalili inayojulisha kuwa ´Aliy anaonelea kuwa hukumu ni yenye kuthibiti hata baada ya kufa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni jambo lisilowezekana jambo likafutwa baada ya kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mash ´alaal-Khuffayn, katika Madjmuu´-ul-Fataawaa (11/158)
  • Imechapishwa: 17/04/2020