2 – Imaam na ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah)

Aliulizwa (Rahimahu Allaah) kuhusu Shaykh Rabiy´ bin Haadiy na Shaykh Muhammad Amaan. Akajibu ifuatavyo:

“Ama kuhusu watu hawa wawili waheshimiwa, Shaykh Muhammad Amaan al-Jaamiy na Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy, wote wawili ni katika Ahl-us-Sunanh. Ninawajua  vyema kwa elimu, fadhila na ´Aqiydah sahihi. Dr. Muhammad Amaan (Rahimahu Allaah) amekufa usiku wa kuamkia alkhamisi tarehe ishirini na saba Sha´baan mwaka huu. Ninashauri kustafidi kutoka kwenye vitabu kwao. Ninamuomba Allaah Awawafikishe wote katika Anayoyaridhia, Amsamehe Shaykh Muhammad Amaan aliyekufa na Awawafikishe Waislamu wote katika radhi Zake na wema wao – hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia, Aliye karibu.”[1]

Kadhalika amesema:

“Shaykh Rabiy´ ni katika wabora wa Ahl-us-Sunnah. Anajulikana vyema kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah. Vitabu na makala zake vinajulikana.”[2]

Amesema pia:

“Hatuna mashaka yoyote na ndugu zetu wanachuoni wanaojulikana al-Madiynah. Wana ´Aqiydah nzuri na ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Miongoni mwao ni Shaykh Muhammad Amaan biy ´Aliy, Shaykh Rabiy´ bin Haadiy, Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy, Shaykh Faalih Naafiy´ na Shaykh Muhammad bin Haadiy. Wote hawa wanajulikana kwetu kuwa na msimamo mzuri, elimu na ´Aqiydah nzuri. Lakini, walinganizi wa batili wanawinda katika maji machafu. Wao ndio wanawashawishi watu na kuzungumzia mambo haya. Wanasema makusudio ni haya na yale. Sio jambo zuri. Lililo la wajibu ni kuyafasiri maneno kwa njia nzuri iwezekanayo.”[3]

Baada ya Shaykh kutoa muhadhara kwa anwani “at-Tamassuk bil-Manhaj as-Salafiy”, akasema (Rahimahu Allaah):

“Tumesikia sote maneno haya yaliyobarikiwa na mazuri kutoka kwa muheshimiwa Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy, mada kuhusiana na kushikamana barabara na Qur-aan na Sunnah na kutahadharisha na yale yanayokwenda kinyume navyo, mgawanyiko na kasumba ya matamanio. Amefanya vyema, vizuri na amefaidisha wengine. Allaah Amjaze kheri na Amlipe maradufu.”

Katika kanda hiohio amesema tena:

“Aliyosema muheshimiwa Shaykh Rabiy´ kuhusu Da´wah ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah), ni kweli. Hakika Allaah Ameuneemesha mji huu kwa Da´wah hii iliyobarikiwa, nayo ni Da´wah ya Salafiyyah. Lakini maadui wameipa sura mbaya Da´wah hii na kusema:

“Wahhaabiyyah na watu wa Bid´ah. Wamefanya haya na yale.”

Uhakika wa mambo ni kwamba ni wapotevu na ni watu wa Bid´ah. Ima ni wajinga au anamfuata kichwa mchunga mjinga mwengine. Ima ni wajinga, anamfuata kichwa mchunga mjinga mwengine au anafuata matamanio yake ambaye anamuasi Allaah kwa ujuzi. Hawa ndio maadui wa Da´wah ya Salafiyyah. Ima ni mjinga, anamfuata kichwa mchunga mjinga au ni mwenye kufuata matamanio ambaye anashabikia matamanio yake ambaye anataka kula na kuwaridhisha watu kwa mujibu wa tumbo lake na matamanio yake.”

Amesema pia katika muhadhara huohuo:

“Ninamuomba Allaah Amuwafikishe muheshimiwa Shaykh Rabiy´ katika kila kheri na Amlipe kheri kwa maneno yake.”

Shaykh Rabiy´ alimtumia kitabu chake “Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Naqd-ir-Rijaal wal-Kutub wat-Twawaaif” Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz, akakituma kwa Shaykh ´Abdul-´Aziyz ar-Raajihiy. Baada ya Shaykh ar-Raajihiy kujibu, Shaykh Ibn Baaz akaandika barua hii kwa Shaykh Rabiy´:

“Kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz kwenda kwa muheshimiwa ndugu, Dr. Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy – Allaah Amuwafikishe kwa yale yanayomridhisha na Amzidishie elimu na imani yake. Aamiyn! Salaamun ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh.

Amma ba´d:

Ninakufikishia jibu la muheshimiwa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy kuhusu kitabu chenu “Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Naqd-ir-Rijaal wal-Kutub wat-Twawaaif”, kwa kuwa nilimwacha yeye afanye hilo kutokana na kutokuweza kwangu mimi kufanya hivo. Amejibu kwa mujibu wa aliyoyaona humo. Jibu lake limenifurahisha na himdi zote njema ni za Allaah. Ninamuomba Allaah Atujaalie sisi, nyinyi na ndugu zetu wengine kuwa katika walinganizi wa uongofu na wenye kuinusuru haki.”[4]

Shaykh na ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy amesema katika kitabu chake “Izhaaq Abaatwil ´Abdil-Latwiyf Baashmiyl”:

“Nilimtembelea Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah). Akaninasihi kumraddi kila anayeenda kinyume na haki na Sunnah. Ni uzuri, ukubwa na uwajibu wa nasaha ilioje kwa yule anayeweza kuitekeleza.”[5]

Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah) alikuwa na uaminifu kwa Shaykh Rabiy´ kiasi cha kwamba wakati mwingine anamuuliza kuhusiana na baadhi ya watu na mifumo yao. Alikuwa akimtumia barua kuhusu maudhui hii. Miongoni mwa barua hizo ni pamoja na zifuatazo:

1- Nambari. 02/352 tarehe 07/02/1413 H:

Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

Kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin Baaz kwenda kwa ndugu muheshimiwa Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy, mwalimu katika Chuo Kikuu cha Kiislamu (Wafaqahu Allaah):

Salaamun ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh.

Wa Ba´d:

Nimefikiwa na khabari kwamba umeandika kitu kuhusu Ustadh Abul-A´laa al-Mawduudiy (Rahimahu Allaah). Naomba unipe nakala juu ya yale uliyoandika katika hayo.

Namuomba Allaah Aniwafikishe mimi na wewe katika yale anayoyapenda na kuyaridhia na Amsaidie kila mmoja katika kila kheri. Hakika Yeye ndiye mbora wa kuombwa…

Wa as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh.

Raisi mkuu wa idara ya mambo ya utafiti ya kielimu na mambo ya kufutu na Da´wah na maelekezo.

2- Nambari. 01/1744 tarehe 25/05/1415 H:

Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

Kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz kwenda kwa ndugu muheshimiwa Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy – Allaah amuwafikishe katika kila kheri:

Salaamun ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh.

Wa Ba´d:

Naomba unitumie nakala ya karatasi inayohusiana na ndugu… Nataraji utamfuatilia kisha utatoa faida kuhusu yale unayoyajua juu ya hali yake ili tuyatendee kazi – Allaah akitaka.

Allaah Atuwafikishe sisi na wewe katika yale Anayoyapenda na kuyaridhia na Abariki katika juhudi zako. Hakika Yeye ndiye mbora wa kuombwa.

Wa as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh.

Muftiy wa Saudi Arabia na raisi wa baraza la Kibaar-ul-´Ulamaa na idara ya mambo ya utafiti ya kielimu na mambo ya kufutu.

3- Nambari. 01/2203 tarehe 24/07/1415 H:

Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

Maudhui: Kuhusu maongezi ya mtu anayeitwa “Naziyh Hammaad” katika Redio ya Qur-aan tukufu:

Kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz kwenda kwa ndugu muheshimiwa Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy – Allaah amsalimishe – Aamiyn!

Salaamun ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh.

Amma Ba´d:

Nimeelezwa na Dr. Muhammad bin Sa´d ash-Shuway´ir ya kwamba umemsikia maongezi kupitia redio ya Qur-aan al-Kariym Naziyh Hammaad siku ya 1415-06-12 baina ya saa 7-8 asubuhi akipindisha maana ya sifa ya haya na sifa ya kughadhibika kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Kwa ajili hiyo, ninataraji kwa kutarajia ujira kutoka kwa Allaah umraddi na kuwawekea haki wazi Waislamu, kwa kuwa mimi sikusikia maongezi hayo. Allaah Akuwafikishe katika kila kheri na Akulipe maradufu. Hakika Yeye ni Mwenye Kusikia na Yu karibu.

Wa as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh.

Muftiy wa Saudi Arabia na raisi wa baraza la Kibaar-ul-´Ulamaa na idara ya mambo ya utafiti ya kielimu na mambo ya kufutu.

Tazama hisia hizi za kidugu na uaminifu wa hali ya juu ambao unafahamisha kwamba Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz alikuwa akimtambua muheshimiwa Shaykh Rabiy´ na elimu yake na kwamba ni mkweli katika yale anayoyasema.

Mimi mwenyewe nilimsikia Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) kwa masikio yangu akimwambia Shaykh Rabiy´:

“Ee Shaykh Rabiy´, mraddi kila mwenye kukosea. Mraddi Ibn Baaz lau atakosea na mraddi Ibn Ibraahiym lau atakosea.”

Baada ya hapo akamsifia sana – na Allaah ni shahidi juu ya yale ninayoyasema.

Uhakika wa mambo ni kwamba Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz alimruhusu afundishe kwenye msikiti wake miezi kadhaa kabla ya kufa kwake. Hii ni dalili inayoonesha kwamba amekufa ilihali yuko radhi na yeye.

Kama ambavyo Shaykh Rabiy´ alikuwa ni mmoja katika wanafunzi wakubwa na wa mwanzonimwanzoni wa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz.

[1] Kanda ”al-Is-ilah as-Swiydiyyah”

[2] Kanda ”Thanaa´-ul-´Ulamaa´ ´alaa as-Shaykh Rabiy´” Tasjiylat Minhaaj-us-Sunnah.

[3] Kanda ”Tawdhwiyh-ul-Bayaan”.

[4] Tazama Utangulizi wa ”Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Naq-ir-Rarijaal wal-Kutub wat-Twawaaif” na “an-Naswr al-´Aziyz ´alaa ar-Radd al-Wajiyz”.

[5] Uk. 104

  • Mhusika: Shaykh Khaalid bin Dhwahwiy adh-Dhwafayriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.rabee.net/ar/sharticles.php?cat=12&id=57
  • Imechapishwa: 28/11/2019