01- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Je, niwaambieni bora ya matendo yenu ambayo yametakasika zaidi kwa Mfalme Wenu na yaliyo juu kabisa katika daraja zenu na ni bora kwenu kuliko kutoa dhahabu na fedha na kukutana na maadui zenu ili kukata shingo zao na wao kukata shingo zenu?” Wakasema: “Ndio, ewe Mtume wa Allaah.” Akasema: “Kumdhukuru Allaah.”

02- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wametangulia Mufarriduun.” Wakauliza: “Ni kina nani Mufarriduun, ewe Mtume wa Allaah?”Akajibu: “Wanaume na wanawake wanaomdhukuru Allaah sana.”

03- ´Abdullaah bin Busr ametaja ya kwamba kuna mtu aliyesema:

“Ewe Mtume wa Allaah! Hakika Shari´ah ya (mambo ya) imani yamekuwa ni mengi kwangu. Nieleze kitu ambacho kila siku naweza kukifanya.” Akasema: “Usiache ulimi wako kila siku kuwa na unyevu kwa kumdhukuru Allaah.”

04- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mfano wa yule anayemdhukuru Allaah na yule asiyemdhukuru Allaah ni kama mfano wa aliye hai na maiti.”

05- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kukaa mahala pasina kumdhukuru Allaah (Ta´ala) hapo, anapata madhara kutoka kwa Allaah (Ta´ala). Mwenye kulala pasina ya kumdhukuru Allaah (Ta´ala) hapo, anapata madhara kutoka kwa Allaah (Ta´ala).”

yaani upungufu, kufuatiwa na mambo mabaya na khasara.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 19/03/2017