19. Yanayomlazimu mwenye istihaadhah katika hali ya utwahara wake

1 – Ni lazima kwake kuoga wakati inapoisha hedhi yake inayozingatiwa kwa mujibu wa vile tulivyobainisha.

2 – Wakati wa kila swalah ataiosha tupu yake ili kuondosha vile vyenye kutoka na ataziba kwa pamba au kitu kingine mfano wake kitachozuia vile vyenye kutoka na atafunga juu yake kitu chenye kuzuia ile pamba isije kudondoka. Halafu atatawadha kila kunapoingia wakati wa kila swalah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu mwanamke mwenye damu ya ugonjwa:

“Wacha kuswali zile siku za hedhi kisha ataoga na atatawadha kwa kila swalah.”

Ameipokea Abu Daawuud, Ibn Maajah na at-Tirmidhiy ambaye amesema:

“Hadiyth ni nzuri.”

 Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Nakusifia pamba ambayo utaweka pale mahali.”

Mtu anaweza vilevile kutumia vitu mbalimbali vya kujihifadhi vinavyopatikana hii leo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 36-37
  • Imechapishwa: 29/10/2019