19. Wanajibidisha juu ya uongozi na kupuuzia ´Aqiydah

19- Wanajibidisha kufikia uongozi. Wanatumia fursa kwa nembo zao ili kwa njia zote waweze kuhudumia mfumo wao. Kwa ajili hiyo utawaona namna ambavyo wanapambana tu na watawala ambao wao wanaonelea kuwa ni washirikina katika Haakimiyyah[1]. Hawajali shirki inayofanywa katika ´ibaadah ambayo Mitume wote ndio walianza kupambana nayo na kuwalingania watu kujiepusha nayo. Mmoja wao alisema pindi alipokuwa akiwaraddi Salafiyyuun:

“Tupeni amani na shirki ya wamaiti, imeshatokomea. Ni juu yetu kupambana na shirki ya waliohai.”

Akimaanisha watawala.[2]

[1] Neno “Haakimiyyah” ni ibara ya ki-Bid´ah ambayo mara nyingi hutumiwa na Qutbiyyuun na vifaranga vyao.

[2] Imaam Swaalih al-Fawzaan amesema:

“Kijitabu hichi kilichoko mbele yetu kimeandikwa na ndugu yetu Shaykh Zayd bin Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy. Kinatahadharisha mifumo hii, kinabainisha athari zake mbaya na kinahimiza kushikamana barabara na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Allaah amjaze kheri na anufaishe kwa nasaha na maelekezo yake.” (Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 7)

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 24
  • Imechapishwa: 25/03/2017