19. Wakati wa kumwingilia mwenye hedhi anapotwahirika

17- Ni lini inajuzu kumwingilia wakati anapotwahirika?

Atapotwahirika kutoka katika hedhi yake na damu yake ikawa imesimama basi hapo itafaa kwake kumwingilia baada ya yeye kuosha ile sehemu ya damu tu, kutawadha au kuoga. Atapofanya moja katika mambo hayo basi itakuwa inajuzu kwa mume kumwingilia[1] kutokana na manneo Yake (Tabaarak wa Ta´ala) katika Aayah iliyotangulia:

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ

“Wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: “Hiyo ni dhara, hivyo basi waepukeni wanawake katika hedhi. Wala msiwakaribie kujimai nao mpaka watwaharike. Hakika Allaah anapenda wenye kutubia na anapenda wenye kujitwaharisha.”[1]

“Wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: “Hiyo ni dhara, hivyo basi waepukeni wanawake katika hedhi. Wala msiwakaribie kujimai nao mpaka watwaharike.”[2]

[1] Haya ndio madhehebu ya Ibn Hazm (10/81), amepokea pia ´Atwaa´ na Qataadah ambaye amesema kuhusiana na mwenye hedhi pindi atapotwahirika:

“Aoshe tupu yake na akutane na mume wake.”

Haya ni madhehebu vilevile ya al-Awzaa´iy kama ilivyo katika “Bidaayat-ul-Mujtahid” (01/44). Ibn Hazm amesema:

“Tumepokea kutoka kwa ´Atwaa´ ya kwamba pindi atapoona amesafika basi atawadhe wakati wa kukutana na mume wake. Haya ndio maoni vilevile ya Abu Sulaymaan na wenzetu wote.”

[2] 02:222

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 120-122
  • Imechapishwa: 12/03/2018