19. Tanbihi ya tatu katika al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar

Tanbihi ya tatu ni kwamba lengo langu kwa kitabu hichi ni wanateolojia wa Raafidhwah wa zamani ambao wameunda fikira za Raafidhwah ambazo zinaubomoa Uislamu kuanzia kwenye msingi wake na kuunda misingi yenye kuharibu ili kuuvunja Uislamu na wabebeji wake kutoka kwenye karne na watu bora baada ya Maswahabah, nao ni Maswahabah watakatifu wa Muhammd (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao Allaah amemchagulia nao Mtume Wake wa mwisho (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili kumnusuru, kufikisha ujumbe wake na kuueneza kwa ulimi, hekima, ubainifu, panga na mikuki. Wakaijaza dunia kwa uadilifu, imani na tabia kwa sura isiyokuwa na mfano katika historia ya uanaadamu.

Lengo langu kwa kitabu hichi ni matusi ya maadui zao. Nitabainisha vitimbi vyao, njama zao na uongo wao juu ya Allaah na Kitabu Chake kisichoingiliwa na batili kwa mbele na kwa nyuma yake.

Mmoja katika maadui hawa ambaye ameivamia Qur-aan kwa upotoshaji na uongo na Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa matusi, kuwachafua na kuwakufurisha ni ´Aliy bin Ibraahiym al-Qummiy. Ameandika kitabu kinachojulikana kwa jina “Tafsiyr al-Qummiy”. Amekufa 307.

Mwingine ni baba yake na mwalimu wake katika upotoshaji na uongo.

Miongoni mwa watu hawa ni yule ambaye amehakiki “Tafsiyr al-Qummiy na anaitwa at-Twayyib al-Muusawiy al-Jazaairiy. Si hata mzuri (Twayyib). Yuko mbali kabisa na watu wazuri! Amepetuka mipaka kwa al-Qummiy na kumnyanyua mpaka angani, kama utakavyoona kwenye utangulizi wa ki-Raafidhwiy wa kitabu chake. Mfano wa upetukaji wake mipaka ni maneno yake:

“Ni miongoni mwa Tafsiyr tukufu zinazofichua Aayah zilizoteremshwa juu ya watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Ukweli wa mambo ni kwamba al-Qummiy na mwalimu wake wamezusha Aayah hizi kwa watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuichafua Qur-aan kwa uzushi huu unaokataliwa na Qur-aan na waumini katika kila zama.

Lengo langu kwa kitabu hichi ni an-Nadhr bin Muhammad bin Mas´uud al-´Ayyaashiy ambaye ameandika Tafsiyr inayojulikana kwa Raafidhwah. Amekufa 320.

Lengo langu ni uongo wake kwa mwalimu na Haashim ar-Rasuuliy al-Mahlaatiy ambaye amehakiki kitabu chake na wale walionukuu uongo wa kitabu hichi juu ya Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), upotoshaji wa Qur-aan na matusi kwa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama mfano wa al-Majlisiy ambaye ni mwandishi wa “Bihaar-ul-Anwaar”, al-Hurr al-´Aamiliy ambaye ni mwandishi wa “Wasaa-il-us-Shiy´ah”, Hishaam al-Bahraaniy ambaye ni mwandishi wa “al-Burhaan” na al-Faydhw al-Kaashaaniy ambaye ni mwandishi wa “as-Swaafiy”.

Lengo langu ni Muhammad bin Ya´quub al-Kulayniy ar-Raaziy ambaye amefariki 328-329. Ni mwandishi wa “al-Kaafiy”. Lengo langu ni mhakiki wa kitabu hichi ´Aliy Akbar al-Ghifaariy na wengine wote wenye dini yao na kufuata njia yao kwa kuwakufurisha Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuamini uongo wa viongozi wao juu ya upotoshaji wa Qur-aan na kuwadhulumu watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwapora uongozi.

Ninawakusudia watu wote hawa. Ninaitakidi kuwa ni makafiri wanafiki. Wanachuoni wa Kiislamu wamemkufurisha yule mwenye kuwakufurisha Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tusemeje kwa yule ukiongezea juu ya hilo ana ´Aqiydah yao na mengi chungumzima kama upotoshaji wa Qur-aan na mengine niliyoona na ambayo wewe pia utayaona katika safari hii.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 45-47
  • Imechapishwa: 19/03/2017