19 – Sayyid Qutwub anaraddi Wahdat-ul-Wujuud katika “al-Muqawwamaat”

Shaykh Bakr amesema:

“Nakuzidishia ya kwamba katika kitabu chake “Muqawwamaat-ut-Taswawwur al-Islaamiy” amewaraddi vya kutosha watu wenye nadharia ya kwamba viumbe wote ni Allaah. Kwa ajili hiyo tunamuomba Allaah amsamehe Sayyid kwa maneno yake yasiyokuwa ya wazi. Maneno yake yasiyokuwa ya wazi hayawezi kukabiliana na maneno yake ya wazi na ya kukata. Hivyo natumai kuwa Takfiyr hii[1] isiyokuwa ya moja kwa moja ya Sayyid (Rahimahu Allaah) itaondoshwa. Mimi nakujali.”

1- Mara nyingi sana nimetafuta radd hii ya kutosha juu ya nadharia hii katika kitabu kilichotajwa pasi na kupata kitu[2]. Kama kweli wewe umeyaona basi ni kwa nini hukumnukuu ili hoja yako iwe na nguvu zaidi na ili niondoshe maneno yangu?

2- Ni kwa nini wachapishaji vitabu hawakukichapa kitabu hiki kikubwa kinachomtakasa Sayyid Qutwub kutokamana na nadharia hii? Wamesubiri kati ya miaka kumi na tano mpaka ishirini kabla ya kukichapisha. Hawana haki yoyote ya kueneza batili hizi bila ya kutangaza yaliyomo kwenye “Muqawwamaat-ut-Taswawwur al-Islaami”. Bali angalau kwa uchache ilikuwa ni wajibu kwao kuweka taaliki katika maneno ya Sayyid ya khatari katika “al-Hadiyd”, “al-Ikhlaasw” na “al-Kawthar” kwa radd hii ya kutosheleza.

3- Kutoyaweka hadharani linatufanya sisi kuzidi kuyakinisha zaidi kutokuwepo kwake kabisa katika “Muqawwamaat-ut-Taswawwur al-Islaami”.

[1] Sikumfanyia Sayyid Qutwub Takfiyr si ya moja kwa moja wala isiyokuwa ya moja kwa moja.

[2] Uhakika wa mambo ni kuwa hapa pia Sayyid katika baadhi ya sehemu anazunguka katika nadharia ya kwamba viumbe wote ni Allaah na ya kwamba Allaah amekita na amechanganyika katika kila kitu.