19. Njia ya kumi: kustafidi na njia za kisasa

Miongoni mwa njia za kuifikia elimu ni mwanafunzi kupupia zile njia za kustafidi na elimu kwa sura zake zote. Miongoni mwa njia hizo:

1- Apupie kuhudhuria mizunguko ya kielimu. Hii ndio ambayo as-Salaf as-Swaalih walikuwa wakiitumia katika kujifunza elimu.

2- Miongoni mwa neema za Allaah kwa mwanafunzi hii leo ni kufungua njia mpya ambazo kwazo anaweza kutafuta elimu. Katika njia hizo ni mwanafunzi kuchukua darsa za kielimu zenye faida kutoka kwenye mikanda iliyorekodiwa. Leo mwanafunzi anaweza kujifunza kupitia kwa mwanachuoni ambaye kishakufa, anaweza kujifunza ilihali yuko chumbani kwake na anaweza kujifunza ilihali amekaa nyumbani kwake. Kidokezo! Mwanafunzi atapochukua njia hii hatakiwi kuifanya kuwa ni yenye kutosheleza na mizunguko ya kielimu. Afanye zote mbili kwa pamoja. Kitu cha kwanza ni mizunguko ya wanachuoni. Kisha aambatanishe hilo pamoja na mizunguko ya kielimu. Kwa sharti atangamane nayo kama ambavyo mwalimu anatangamana nae. Achukue darsa na kumfuatilia mwalimu. Afungamanishe na kitabu chake yale anayostafidi kutoka kwenye mkanda. Katika kufanya hivo kuna kheri kubwa na faida nyingi.

3- Katika hayo vilevile ni zile darsa za elimu na zenye faida zinazotolewa kwenye tovuti za intaneti. Ndani yake mna darsa nzuri nzuri. Mwanafunzi anatakiwa pindi anapopata wakati afaidike nazo na akimbilie kustafidi nazo. Kwa sharti zisimtosheleze na mizunguko ya elimu na kutafuta elimu vilevile kutoka kwa wanachuoni. Kwani hakika kuchukua elimu moja kwa moja kutoka kwa wanachuoni ndio asli katika njia ya kutafuta elimu.

 

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Ilm wa Wasaaailuh wa Thimaaruh
  • Imechapishwa: 22/10/2016