19. Ni nani imesuniwa kwake kuomba du´aa ya kuonekana kwa mwezi mwandamo?

Swali 19: Kumepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) du´aa maalum kwa ambaye ameona mwezi mwandamo? Je, inafaa kwa ambaye amesikia khabari za kuandama kwa mwezi kuomba du´aa hiyo japokuwa yeye mwenyewe hakuona mwezi huo?

Jibu: Ndio, aseme:

الله أكبر. اللهم أهله علينا بالأمن والإيمان.. والسلامة والإسلام.. والتوفيق لما تحبه وترضاه. ربي وربك الله. هلال خير ورشد

”Allaah ni mkubwa! Ee Allaah! Uanzishe kwetu kwa amani na imani, usalama na Uislamu, kutuwafikisha kwa yale unayoyapenda na kuyaridhia, Mola wetu na Mola wako ni Allaah. Mwezi mwandamo wa kheri na uongofu.”

Kumepokelewa juu ya hilo Hadiyth mbili kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambazo zimetiwa dosari kidogo. Udhahiri wa Hadiyth ni kwamba mtu asiombe kwa du´aa hii isipokuwa tu pale ambapo atauona mwezi mwandamo. Ama yule ambaye amesikia taarifa yake na hakuuona haikusuniwa kwake kusema hivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 21-22
  • Imechapishwa: 16/04/2021