19. Mwenye busara na namna anavyowajali ndugu na jamaa


1- Ibn-ul-Hanafiyyah amesema:

“Hana hekima yule asiyeishi kwa wema na mshirika wake. Atafanya hivo mpaka pale Allaah atapompa faraja au njia ya kutokea.”

2- Yule anayetaka kuishi na watu vile alivyo atakuja kuyachafua maisha yake na atakosa mapenzi ya kweli. Kwa kuwa mapenzi ya watu hayapatikani kwa njia nyingine isipokuwa kwa kuwasaidia isipokuwa tu ikiwa kama itakuwa inahusiana na madhambi. Hata hivyo ikiwa inahusiana na maasi hakuna usikivu wala utiifu. Watu wameumbwa na matamanio na tabia mbalimbali. Kama jinsi unaona ugumu kuacha tabia ulizoumbiwa kwazo kadhalika wengine wanaona kuwa ni vigumu kuacha tabia walizoumbiwa kwazo. Hakuna njia nyingine ya kupata mapenzi yao safi isipokuwa kwa kuenda nao na kupuuza makosa yao hapa na pale.

3- al-Hasan al-Baswriy amesema:

“Ee mwanaadamu! Tangamana na watu vile unavyotaka – na wao watatangamana na wewe kwa njia hiyo hiyo!”

4- Anayetaka kuwaridhisha watu wote anataka kitu asichoweza kufanikiwa. Lakini mwenye busara anatakiwa kuhakikisha anamridhisha yule anayeshirikiana naye maishani hata kama itakuwa inahusiana na kupenda asichokipenda au kinyume chake maadamu haihusiana na madhambi.

5- Mu´aadh bin Sa´d al-A´war amesema:

“Nilikuwa nimekaa kwa ´Atwaa´ bin Rabaah akaja mwanaume mmoja na kuzungumza. Wakati alipokuwa akizungumza akasimama na kwenda zake. ´Atwaa´ akakasirika na kusema: “Hii ni tabia gani? Mwanaume huyu anazungumza kitu ambacho mimi nina ujuzi nacho zaidi lakini pamoja na hivyo namuonyesha kana kwamba sijui lolote kuhusu jambo hilo.”

6- Abud-Dardaa´ alimwambia Umm-ud-Dardaa´:

“Nikikasirika basi fanya niweze kuwa na furaha.  Ukikasirika nitafanya uwe na furaha. Tusipofanya hivo basi tutafarikiana kwa haraka sana.”

7- Ikitokea mwenye busara kupata usuhubiano wa ambaye hawezi kuamini urafiki wake au urafiki wa ambaye hawezi kuamini udugu wake na akaona kutoka kwao makosa na akawatupilia mbali kwa sababu ya makosa yao, basi atabaki mwenyewe bila ya rafiki yeyote. Anatakiwa kupuuzia kosa la rafiki yake wa kweli na asichukulie kosa la rafiki yake. Mijadala inapelekea kusahihisha zaidi ile mizizi ya mapenzi kuliko yale matawi yake.

8- Ibn Shawdhab amesema:

“Kuna mwanaume alikuwa na mjakazi na siku moja akawa amemjamii kwa siri. Halafu akaenda kwa mke wake na kumwambia: “Maryam alikuwa akioga kila usiku huu. Na wewe pia oga!” Kisha akaoga yeye na mke wake. Maryam akawa anaoga kila usiku.”

9- Abu Saa-iyb amesema:

“Usitaamiliane kwa hadaa. Hadaa ni tabia ya wenye madhambi. Mpe ndugu yako nasaha za kweli sawa ziwe ni nzuri au mbaya. Msaidie kwa kila hali na potea naye pindi anapopotea.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 70-72
  • Imechapishwa: 06/02/2018