19. Mke anatakiwa kuwa mwenye shukurani kwa mume wake

Miongoni mwa haki za mume juu ya mke wake ni yeye kumshukuru kwa yale anayomfanyia na asikufuru neema. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah Hamtazami mwanamke asiyemshukuru mume wake na yeye hawezi kujitosheleza naye.”[1]

Mke mwema alobarikiwa anachelea kutoonyesha shukurani kwa mume wake. Anailea nafsi yake na kujilaumu kwa kutoonyesha shukurani kwa mume wake. Kwa nini? Ndio, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimeona Moto na mpaka hivi leo sijaona kitu kama hicho. Niliona wakazi wake wengi walikuwa ni wanawake.” Wakasema: “Ni kwa sababu gani, ewe Mtume wa Allaah?” Akasema: “Kwa kutoonyesha kwao shukurani.” Wakasema: “Hawana shukurani kwa Allaah?” Akasema: “Hawaonyeshi shukurani kwa waume na kutendewa vizuri. Lau utamtendea mmoja wao wema mwaka mzima na halafu katika tokeo fulani akaona kitu kwako, atasema: “Katu sijaona wema wowote kutoka kwako.”[2]

[1] an-Nasaaiy (5/9135), al-Haakim (2/2771) na al-Bazzaar (6/2349). Mnyororo ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Haakim. Hadiyth ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (289).

[2] al-Bukhaariy (1052) na Muslim (907).

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 32
  • Imechapishwa: 24/03/2017