19. Mjamzito anayechelewesha Ramadhaan mwenye kupata dhambi na asiyepata dhambi


Swali 19: Mwanamke amekula siku saba katika Ramadhaan akiwa na damu ya uzazi na hakuwahi kulipa mpaka akaingiliwa na Ramadhaan ya pili. Ramadhaan ya pili ikamkuta akiwa ni mwenye kunyonyesha kwa muda wa siku saba na hakuweza kulipa kwa hoja ya kunyonyesha. Ni kipi kinachomlazimu?

Jibu: Ikiwa mwanamke huyu mambo ni kama alivyojieleza mwenyewe ya kwamba ni mgonjwa na hakuweza kulipa, basi pindi tu atakapoweza basi atafunga. Ni mwenye kupewa udhuru hata kama amefikiwa na Ramadhaan ya pili.

Lakini akiwa hana udhuru wowote na si vinginevyo isipokuwa anatafuta vijisababu na kupuuza basi haifai kwake kuchelewesha kulipa Ramadhaan mpaka akaingiliwa na Ramadhaan ya pili. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Nilikuwa nadaiwa funga na nashindwa kuilipa mpaka katika Sha´baan.”

Kutokana na haya mwanamke huyu anatakiwa kuitazama nafsi yake mwenyewe; akiwa hana udhuru wowote basi anapata dhambi. Hivyo itambidi atubu kwa Allaah na aharakishe kulipa ile dhimmah ya swawm inayomlazimu. Akiwa ni mwenye udhuru hakuna dhambi juu yake hata kama itapelekea akachelewa mwaka mmoja au miwili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 02/07/2021