Madhambi yakikithiri, basi moyo wa huyo mtenda dhambi hufunga. Katika hali hii anakuwa katika waghafilikaji. Baadhi ya Salaf wamesema kuhusiana na maneno ya Allaah (Ta´ala):

كَلَّاۖ بَلْۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ

“Sivyo hivyo! Bali imefanya kutu juu ya nyoyo zao yale waliyokuwa wakiyachuma!”[1]

“Ni madhambi baada ya madhambi.”

al-Hasan al-Baswriy amesema:

“Ni madhambi yaliyopandiana mpaka yanaufanya moyo kuwa kipofu.”

Wengine wakasema:

“Pindi yalipokithiri madhambi na maasi yao, nyoyo zao zikawazunguka.”

Msingi wa haya ni kuwa moyo unaharibiwa kwa madhambi. Yakizidi kuwa mengi, kuharibika kunazidi mpaka hatimaye yanauteketeza moyo. Baadaye yanaendelea mpaka moyo unafungika tena. Kwa ajili hiyo moyo unafungika. Hayo yakipitika baada ya uongofu na ujuzi, unaenda kinyume na unapindishwa juu chini. Hapo ndipo anaumiliki adui na anauelekeza kule anakotaka.

[1] 83:14

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 72
  • Imechapishwa: 09/01/2018