133- an-Nawwaas bin Sam´aan ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“´Iysaa bin Maryam atashuka kwenye mnari mweupe Dameski.”

Katika upokezi mwingine imekuja:

“… kwenye mnara… “

Hiki ni kipande cha Hadiyth ndefu ambapo ametajwa vilevile ad-Dajjaal na Ya´juuj na Ma´juuj. Muslim ameipokea katika “as-Swahiyh” yake kwa ukamilifu wake.

134- Ka´b-ul-Ahbaar amesema:

“´Iysaa atashuka kwenye mnara karibu na mlango wa mashariki wa Dameski. Halafu aende na waislamu wake kuelekea Yerusalemu.”

Kuna Hadiyth zinazozungumzia ya kwamba ´Iysaa atashuka Yerusalemu, lakini milolongo ya wapokezi wake haina nguvu. Na kama zitakuwa ni Swahiyh basi maana yake ni kwamba yeye pamoja na waumini ataokuwa nao watafika Dameski wakiwa ni wenye kutokea Dameski. Hivyo ndivyo alivyosema ´A´ish na Ka´b kwa ajili ya kuoanisha Hadiyth zote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Baghdaadiy al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-ush-Shaam, uk. 146-149
  • Imechapishwa: 10/02/2017