19. Inafaa kusikiliza mikanda ya Salmaan al-´Awdah, Safar al-Hawaaliy, Sa´iyd al-Qahtwaaniy na ´Aaidh al-Qarniy?

Swali 19: Kuna vijana wengi wanaosikiliza mikanda Salmaan al-´Awdah, Safar al-Hawaaliy, Sa´iyd al-Qahtwaaniy na ´Aaidh al-Qarniy. Je, unawanasihi vijana hawa kusitisha kusikiliza mikanda yao au hapana?

Jibu: Ndio. Kwa sababu mikanda yao inaweza kuwa na mambo wasiyoyajua vijana hawa na hatimaye wakadanganyika nayo. Watu hawa wana maneno yasiyokuwa mazuri. Ni maneno wanayotakiwa kuacha na wajirudi kwayo. ´Aaidh al-Qarniy – Allaah amuwafikishe na amthibitishe – amejirudi katika mambo kumi na saba. Tunatarajia vilevile atajirudi katika makosa yaliyobaki. Amesema:

Swali na ufunge utakavyo

dini haitambui mtu kwa kuswali na kufunga

Wewe ni padiri katika watawa

na sio katika watu wa Muhammad – inatosheleza kulaumika.

Haya ni mashairi ambayo kwa hakika hayatakiwi kusikilizwa. Anaamrisha kuwafanyia uasi watawala. Tunatarajia kuwa amejirudi kwayo.

Mfano wa maneno kama haya, maneno ya Salmaan na baadhi ya maneno ya Safar yanaweza kuwa na makosa ambayo hakuna mwenye kuyajua isipokuwa wanachuoni.

Lililo bora kwa mwanafunzi mwerevu asisikilize mikanda hii.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 16/07/2017