Download

41-

سُبْحَانَ رَبِّيَ الأَعْلَى

“Ametakasika, Mola wangu, Aliye juu.”[1]

mara tatu[2].

42-

سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي

“Kutakasika ni Kwako, ee Allaah Mola wetu, na himdi zote ni Zako. Ee Allaah! Nisamehe.”[3]

43-

سُبُّوُحٌ، قُدُّوسٌ، رَبُّ المَلاَئِكَةِ وَالرُّوحِ

“Mwingi wa kutakaswa, mtakatifu, Mola wa Malaika na roho [Jibriyl].”[4]

44-

اللَّهُمَّ لَكَ سَجَدْتُ وَبِكَ آمَنْتُ، وَلَكَ أَسْلَمْتُ، سَجَدَ وَجْهِيَ لِلَّذِي خَلَقَهُ، وَصَوَّرَهُ، وَشَقَّ سَمْعَهُ وَبَصَرَهُ، تَبَارَكَ اللَّهُ أَحْسنُ الْخَالِقينَ

“Ee Allaah! Kwako nimesujudu, Wewe nimekuamini, Kwako nimejisalimisha, uso wangu umemsujudia Yule ambaye kaumba, akautia sura na akapasua usikizi wake na uoni wake. ametakasika Allaah, mbora wa waumbaji.”[5]

45-

سُبْحَانَ ذِي الْجَبَرُوتِ، وَالْمَلَكُوتِ، وَالْكِبْرِيَاءِ، وَالْعَظَمَةِ

“Ametakasika Mwenye utawala, ufalme, ukubwa na utukufu.”[6]

46-

اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي ذَنْبِي كُلَّهُ: دِقَّهُ وَجِلَّهُ، وَأَوَّلَهُ وَآخِرَهُ، وَعَلاَنِيَّتَهُ وَسِرَّهُ

“Ee Allaah! Nisamehe dhambi zangu zote; ndogo na kubwa, za mwanzo na za mwisho, za dhahiri na za kujificha.”[7]

47-

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِرِضَاكَ مِنْ سَخَطِكَ، وَبِمُعَافَاتِكَ مِنْ عُقوبَتِكَ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْكَ، لاَ أُحْصِي ثَنَاءً عَلَيْكَ، أَنْتَ كَمَا أَثْنَيْتَ عَلَى نَفْسِكَ

“Ee Allaah! Hakika mimi najilinda kwa radhi Zako kutokamana na ghadhabu Zako, kwa msamaha Wako kutokamana na adhabu Yako, naomba hifadhi Kwako, mimi siwezi kukusifu ustahikivo – Wewe ni kama Ulivyojisifu juu ya nafsi Yako.”[8]

[1] Muslim (477).

[2] Wameipokea watunzi wa Sunan, Ahmad, Abu Daawuud (870), at-Tirmidhiy (262), an-Nasaa´iy (1007), Ibn Maajah (897) na Ahmad (3514). Tazama “Swahiyh at-Tirmidhiy” (01/83).

[3] al-Bukhaariy (794) na Muslim (484).

[4] Muslim (487) na Abu Daawuud (872).

[5] Muslim (771) na wengineo.

[6] Abu Daawuud (873), an-Nasaa´iy (1131) na Ahmad (23980). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Abiy Daawuud” (01/166).

[7] Muslim (483).

[8] Muslim (486).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 30/09/2018