19- al-Haakim bin Muhammad bin ´Abdillaah al-Azdiy al-Imaam ametuhadithia kwa kutusomea: Muhammad bin Muhammad al-Anmaatwiy ametuhadithia: Muhammad bin Ayyuub ametuhadithia: Abuul-Waliyd at-Twayaalisiy amenihadithia, kutoka kwa Shu´bah… ح Ahmad bin Hamdaan ametuhadithia: Haamid bin Muhammad ametuhadithia: Muhammad bin Swaalih al-Ashajj ametuhadithia: Daawuud bin Ibraahiym ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia… ح ´Abdul-Jabbaar ametuhadithia: Ibn Mahbuub ametuhadithia: Abuu ´Iysaa ametuhadithia: Muhammad bin Bashshaar ametuhadithia: Muhammad bin Ja´far ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa Qataadah: Nilimsikia Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) akisimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna Mtume yeyote isipokuwa aliutahadharisha Ummah wake juu ya mwongo mwenye chongo. Hakika ana chongo, lakini Mola wenu (´Azza wa Jall) hana chongo. Kati ya macho yake kumeandikwa ك ف ر .”[1]

Matamshi ni ya Ghandar.

[1] al-Bukhaariy (7131) na Muslim (2933).

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 45
  • Imechapishwa: 24/01/2017