19. Dalili ya kumi na saba kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

17- Faatwimah bint Muhammad bin ´Aliy al-Bazzaazah alisomewa huko Nafiysah na huku nikisikiza: Abu ´Abdillaah al-Husayn bin Ahmad bin Muhammad bin Twalhah amekukhabarisheni: Abul-Husayn ´Aliy bin Muhammad bin ´Abdillaah bin Bishraan ametuhadhia: ´Abdus-Swamad bin ´Aliy bin Mukram ametuhadithia: al-Haarith bin Muhammad bin Daahir at-Tamiymiy ametuhadithia: ´Aliy bin ´Aaswim ametuhadithia: Daawuud bin Abiy Hind ametuhadithia, kutoka kwa ´Aamir ash-Sha´biy ambaye amesimulia kwamba Zaynab alikuwa akisema kumwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Katika wake zako wote mimi ndiye nina haki kubwa zaidi na mimi ndiye niliyefungishwa ndoa iliyo bora kabisa. Nilifungishwa ndoa na Mwingi wa huruma kutoka juu ya ´Arshi Yake na Jibriyl ndiye alikuwa mkati kati. Isitoshe mimi ni binamu yako. Hakuna mwingine katika wakezo ambaye ni ndugu isipokuwa mimi tu.”[1]

[1] at-Twabariy (22/14), al-Bukhaariy (7421), at-Tirmidhiy (3213) na Ahmad (3/226).

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 97
  • Imechapishwa: 02/06/2018