Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

14- Mwenye kufisha bila ya khofu yoyote.

MAELEZO

Anawafisha wale waliohai pindi muda wao wa kuishi unapotimia. Hafanyi hivo kwa sababu anawaogopa, anafanya hivo kutokana na hekima Yake (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa sababu maisha ya duniani yana mwisho wake tofauti na maisha ya Aakhirah yasiyokuwa na kikomo. Hawafishi viumbe kwa sababu ya kuwaogopa au kustarehe kutokamana nao. Hata kama watamkufuru Yeye hadhuriki na ukafiri wao – bali wao wenyewe ndio wanajidhuru nafsi zao. Hata hivyo anafurahikia tawbah zao. Kwa sababu anawatamania na kuwapendelea kheri. Hata hivyo hafurahikii tawbah zao kwa sababu ni Mwenye kuzihitajia, bali ni kwa sababu ya upole na uzuri Wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 39-40
  • Imechapishwa: 16/09/2019