19. al-Albaaniy amesema yaleyale yaliyosemwa na Ibn Taymiyyah

Amesema kwamba al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Msingi na lililo bora ni kwamba waislamu wanatakiwa kuwa chini ya kiongozi na uongozi mmoja. Kama hilo haliwezekani, basi itafaa kuwepo kwa watawala wengi kwa kiasi cha haja. Wapewe sehemu ya viapo ili waweze kuwaongoza raia wao kwa mujibu wa kanuni na misingi ya Shari´ah.”

Maneno haya hayamtoi nje ya Salafiyyah. Wanachuoni wana maoni tofauti juu ya hilo. Jengine ni kwamba tofauti katika hayo ni ya kinadharia. Ama uhalisia wa mambo hakuna yeyote (isipokuwa maoni mabovu) aliyesema juu ya kutenguka na kubatilika kwa serikali katika nchi. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

“Kwa mujibu wa ´Aqiydah ni kwamba waislamu wanatakiwa kuwa na kiongozi mmoja tu.  Wengine waliobaki wanatakiwa kuwa manaibu wake. Tukikadiria kutokea kinyume na hayo katika Ummah kwa sababu ya maasi kutoka kwa baadhi yao na waliobaki wakashindwa ambapo ikawa ni sababu ya kuwepo watawala wengi, basi itakuwa ni wajibu kwa kila kiongozi kusimamisha adhabu za Kishari´ah na kutetekeleza haki mbalimbali.”[1]

Bi maana kwa yale yaliyo chini yake. Ni dalili inayoonyesha kuwa al-Albaaniy anasema yaleyale yaliyosemwa na Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (34/175-176).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 01/12/2018