18. Yanayohalalika kwa mume kutoka kwa mwenye hedhi


16- Yanayohalalika kwake kutoka kwa mwenye hedhi

Inajuzu kwake kustarehe na mwenye hedhi – mbali na kumwingilia kwenye tupu. Kuna Hadiyth juu ya hio:

1- Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… fanya kila kitu isipokuwa tendo la ndoa.”

2- ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia:

“Pindi mmoja wetu alipokuwa na hedhi, basi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimwamrisha kufunga kitambaa kisha mume wake anastarehe naye”. Wakati mwingine amesema: “…kisha anamkumbatia na kumpapasa.”[1]

3- Baadhi ya wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wamesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anataka kutoka kwa mwenye hedhi kitu, basi huweka nguo kwenye tupu yake halafu anafanya kila anachotaka.”[2]

[1] Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na Abu ´Awaanah katika “as-Swahiyh” zao, Abu Daawuud na haya ni matamshi yake kwa nambari (260) na ameisahihisha.

[2] Ameipokea Abu Daawuud (262) kutoka katika “as-Swahiyh” yake na siyaaq ni yake, mlolongo wa wapokezi wake ni Swahiyh juu ya masharti ya Muslim, Ibn ´Abdil-Haadiy ameisahihisha. Ibn Hajar na al-Bayhaqiy wameipa nguvu (01/314) na nyongeza ni yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 122
  • Imechapishwa: 12/03/2018