127- Haafidhw Abul-Qaasim amepokea kwa mlolongo wa wapokezi wake kupitia kwa Abud-Dardaa´ ya kwamba alikuwa Dameski na Mu´aawiyah akamuomba arudi Hims. Ndipo akasema:

“Ee Mu´aawiyah! Unaniamrisha kutoka katika msingi wa nyumba ya Kiislamu?”

128- Abu Khaythamah amepokea ya kwamba Mu´aawiyah alimuuliza Ka´b:

“Unapenda zaidi Hims kuliko Dameski?” Akajibu: “Hapana. Dameski.” Akasema: “Kwa nini?” Akasema: “Kijinyumba kidogo Dameski ni bora kuliko nyumba kubwa Hims.”

129- Haafidhw Abul-Qaasim amepokea kupitia kwa Yuunus bin Maysarah bin Halbas ya kwamba kuna mwanamme aliishi yeye na familia yake mwezi mzima Twabariyyah na wakatoshelezwa kwa 6.5 kg. Alipohama Dameski akatoshelezwa kwa 3.25 kg.

130- ´Abdur-Rahmaan bin Yaziyd bin Jaabir amesema:

“Nilimuuliza Sallaam bin al-Aswad sababu ya yeye kuhama kutoka Hims kwenda Dameski. Akasema: “Nimefikiwa na khabari ya kwamba baraka huko zinakuwa ni maradufu.”

131- ´Ubayd bin Ya´laa´ alikuwa ni mwanachuoni mmoja kutoka Yerusalemu anayeishi ´Asqalaan. Alimwambia mwanamme mmoja:

“Hama kutoka Palestina uje Dameski. Baraka za Shaam zote zinaenda Dameski.”

132- Abu Khaythamah amepokea kupitia kwa ash-Shaybah aliyesema:

“Nawf al-Bikaaliy alikuwa imaam wa Dameski. Alipokuwa anawaelekea watu alikuwa akiwaambia: “Allaah asimpende yule asiyewapenda. Allaah asimrehemu yule asiyewarehemu.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Baghdaadiy al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-ush-Shaam, uk. 141-143
  • Imechapishwa: 10/02/2017