18. Wamedangana kutokamana na Uislamu natija ya wenye kufuata kichwa mchunga

´Allaamah Muhammad Sultwaan al-Ma´suumiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Waislamu katika miji ya kijapani huko nchini Tokyo na Osaka waliniuliza swali lifuatalo:

  1. Uislamu ni nini?
  2. Madhehebu ni nini?
  3. Je, ni lazima kwa mtu mwenye kuingia katika Uislamu kufuata moja katika yale madhehehu mane? Ni lazima awe Maalikiy, Hanafiy, Shaafi´iy au kitu kingine?

Tunauliza haya kwa sababu kumetokea tofauti kubwa katika nchi yetu. Wakati kundi la wajapani lilipotaka kuingia katika Uislamu na kutukuzwa kwa imani, lilienda katika shirika la Kiislamu Tokyo. Kundi la wahindi likawaambia kwamba wanatakiwa kuchagua madhehebu ya Abu Haniyfah, kwa kuwa ni taa la Ummah. Kundi la waindonesia kutoka Java likawaambia kwamba wanatakiwa anatakiwa kuwa Shaafi´iy. Pindi wajapani waliposikia haya, wakastaajabu sana na wakadangana. Hatimaye suala hili la madhehebu likapelekea kuzuia watu na Uislamu na hawakusilimu tena.”[1]

[1] Hadiyyat-us-Sultwaan ilaa Muslimiy Bilaad-il-Yaabaan.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 60-61
  • Imechapishwa: 22/01/2019