18. Tanbihi ya pili katika al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar


Tanbihi ya pili ni kwamba nimeona kuwa wakati al-Qummiy anapofasiri Aayah ya Qur-aan husema:

” Amesema…”

Kisha hutaja Aayah. Hasemi “Allaah (Ta´ala) Amesema”, “Allaah (´Azza wa Jalla) Amesema” au “Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Amesema”. Jambo linalompa msomaji hisia ya kwamba mtu huyu hamuadhimishi Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala). Hata hivyo hamtaji yeyote katika maimamu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa husema “´alayhis-Salaam”.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 45
  • Imechapishwa: 19/03/2017