18. Swalah ya jeneza inaanguka kwa ukafiri na kuritadi

5- Ni haramu kumswalia anayeritadi baada ya kufa kwake.

Vilevile ni haramu kumuombea du´aa ya msamaha na rehema. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَا تُصَلِّ عَلَىٰ أَحَدٍ مِّنْهُم مَّاتَ أَبَدًا وَلَا تَقُمْ عَلَىٰ قَبْرِهِ ۖ إِنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَمَاتُوا وَهُمْ فَاسِقُونَ

“Wala usimswalie yeyote kamwe miongoni mwao akifa na wala usisimame kaburini kwake; hakika wao wamemkufuru Allaah na Mtume Wake na wakafa hali wao ni mafasiki.”[1]

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ وَمَا كَانَ اسْتِغْفَارُ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوْعِدَةٍ وَعَدَهَا إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ عَدُوٌّ لِّلَّـهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ ۚ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَأَوَّاهٌ حَلِيمٌ

“Haimpasi Nabii na wale walioamini kuwaombea maghfirah washirikina, japokuwa ni jamaa zao wa karibu, baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa Motoni. Hayakuwa maombi ya Ibraahiym kumuombea baba yake isipokuwa kwa sababu ya ahadi aliyoahidiana naye, lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui wa Allaah alijiepusha naye. Hakika Ibraahiym [alikuwa] ni mwenye huruma mno na mvumilivu.”[2]

Kumuombea msamaha au rehema kafiri, pasi na kujali ukafiri wake, ni kupetuka mipaka katika du´aa, kumfanyia mzaha Allaah na ni kupinda kunako njia ya Mtume na waumini. Ni vipi mtu anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho anaweza kumuombea msamaha na rehema mtu ambaye amekufa katika hali ya kikafiri na alikuwa ni adui wa Allaah (Ta´ala)? Allaah (Ta´ala) amesema:

مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ

“Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake na Mtume Wake na Jibriyl na Miykaala basi [atambue kuwa] Allaah ni adui kwa makafiri.”[3]

Katika Aayah hii Allaah (Ta´ala) amebainisha kuwa Yeye ni adui wa kila kafiri. Lililo la wajibu kwa muislamu ni yeye kujitenga mbali na makafiri wote. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ

“Ibraahiym alipomwambia baba yake na watu wake: “Hakika mimi mwenye kujitoa katika dhima na yale mnayoyaabudu! [Simuabudu mwengine yeyote] isipokuwa Yule aliyeniumba, hakika Yeye ataniongoa.”[4]

قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآءُ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ

“Hakika mna kigezo kizuri kwa Ibraahiym na wale walio pamoja naye, walipowaambia watu wao: “Hakika sisi tumejitenga mbali nanyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah, tunakukanusheni na umedhihirika baina yetu na baina yenu uadui na bughudha milele mpaka mumuamini Allaah pekee.””[5]

Kwa hivyo atakuwa vilevile amehakikisha kumuiga Mtume wa Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأَذَانٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ إِلَى النَّاسِ يَوْمَ الْحَجِّ الْأَكْبَرِ أَنَّ اللَّـهَ بَرِيءٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ ۙ وَرَسُولُهُ

“Na ni tangazo kutoka kwa Allaah na Mtume Wake kwa watu siku ya Hajj kubwa kwamba: “Allaah na Mtume Wake hawana jukumu lolote kwa washirikina.””[6]

Katika mafundo imara kabisa ya imani ni kupenda kwa ajili ya Allaah, kuchukia kwa ajili ya Allaah, kujenga urafiki kwa ajili ya Allaah na kujenga uadui kwa ajili ya Allaah kwa ajili ya kwamba mapenzi yako, kuchukia kwako, kujenga kwako urafiki na kujenga kwako uadui kuwe kunafuata radhi za Allaah (´Azza wa Jall).

[1] 09:84

[2] 09:113-114

[3] 02:98

[4] 43:26-27

[5] 60:04

[6] 09:03

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Hukm Taarik-is-Swalaah, uk. 18-19
  • Imechapishwa: 22/10/2016