18. Riziki yetu iko mbinguni


87- Sa´iyd bin Jubayr au adh-Dhwahhaak amesema kuhusu Kauli ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala):

وَفِي السَّمَاءِ رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ فَوَرَبِّ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِنَّهُ لَحَقٌّ مِّثْلَ مَا أَنَّكُمْ تَنطِقُونَ

“Na katika mbingu, kuna riziki zenu, na yale mnayoahidiwa. Basi Naapa kwa Mola wa mbingu na ardhi, hakika hiyo ni Haki kama mnavyotamka.” (51:22-23)

“Riziki hapa kinachokusudiwa ni mvua na barafu inayoanguka kutoka mbinguni ndio sababu ya uotaji ambao watu wanaishi kwa sababu yake. Dalili ya hilo ni Kauli ya Allaah (Ta´ala):

وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ السَّمَاءِ مِن رِّزْقٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا

“Na kupishana usiku na mchana, na Anayoteremsha Allaah kutoka mbinguni katika riziki, Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake.” (45:05)

Yaani mvua.”

88- Tafsiri nyingine inasema kuwa riziki iko kwenye mvua. Mvua huwa ikiitwa mbingu.

89- Tafsiri nyingine inasema kuwa riziki ni kazi ya Mola wa mbingu. Dalili ya hilo ni:

وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ رِزْقُهَا

“Na hakuna kiumbe chochote katika ardhi isipokuwa riziki yake iko kwa Allaah.” (11:06)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Hirsw biz-Zuhd wal-Qanaa´ah, uk. 65
  • Imechapishwa: 18/03/2017