18. Ni ipi hukumu ya mfungaji kutumia wanja na kujitia manukato?

Swali 18: Ni ipi hukumu mfungaji kutumia wanja na kujitia manukato?

Jibu: Lililo bora ni kuepuka wanja kwa sababu kuna Hadiyth dhaifu juu ya hilo. Ukitumia wanja hakuchukuwi muda mrefu isipokuwa utaanza kutema makohozi. Inatokea wanja unatoa makohozi. Mishipa inanyonya wanja unatembea ndani ya mishipa.

Manukato hayana neno. Manukato yana hukumu moja kama mioshi mingine inayovutiwa pumzi kwa ndani pasi na kukusudia. Maswahabah wa kike (Radhiya Allaahu ´anhunn) walikuwa wakipika chakula na hivyo moshi ilikuwa ni vigumu kuuepuka. Hata hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwakataza hilo. Lau (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) angefanya hivo kungelikuwa kuna uzito kwa Ummah.

Kuhusu sigara, bangi na mabomba ya sigara yanaharibu swawm. Ni katika vichafu na vilevile vinamfanya mfungaji kuwa na nguvu.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 33-35f
  • Imechapishwa: 12/06/2017