18. Misimamo mitatu ya watu juu ya mawalii wa Allaah

Watu katika maudhui haya wamegawanyika makundi matatu; makundi mawili yamechupa mpaka na moja liko kati na kati:

1 – Miongoni mwa watu wako ambao wanapoamini kuwa mtu fulani ni walii wa Allaah basi wanakubaliana naye katika kila anachokidhania kuwa kimezungumzwa na moyo wake kutoka kwa Mola wake. Matokeo yake akajisalimisha na kila atachokifanya.

2 – Miongoni mwa watu wako ambao wanapomuona amesema au amefanya mambo yasiyoafikiana na Shari´ah, basi wanamtoa nje ya uwalii wa Allaah ijapo atakuwa ni mujtahid aliyekosea.

3 – Bora ya mambo ni yale ya kati na kati; bi maana mtu asimfanye amelindwa na kukosea au mwenye kupata dhambi akiwa ni mujtahid aliyekosea. Kwa msemo mwingine ni kwamba asimfuate katika kila anachokisema na wala asimuhukumu ukafiri na ufuska kutokana na ijtihaad yake. Ni lazima kwa watu kuyafuata yale ambayo Allaah amemtumiliza kwayo Mtume Wake…

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 30
  • Imechapishwa: 24/06/2021