Swali: Msikiti mkuu katika kijiji chetu upo katikati na makaburi yanayouzunguka upande wa kaskazini na kusini. Umbali baina yake na upande wa kaskazini ni mita mbili. Vivyo hivyo upande wa kusini ni mita mbili. Makaburi hayo yapo njiani kupanuliwa. Baadhi ya waswaliji –  Allaah awaongoze – wanayafanya makaburi hayo ndio maeneo ya kuegesha magari yao. Ni ipi hukumu ya mfano wa kitendo kama hichi?

Jibu: Hapana neno kubaki kwa msikiti uliotajwa. Desturi za watu imepita kwamba watu wanazika pembezoni na misikiti. Kwa hivyo hicho hakidhuru kitu. Kinacholengwa ni kwamba hapana vibaya kuzika pembezoni na misikiti kwa sababu ni jambo rahisi kwa watu. Wakitoka msikitini wanamzika karibu na msikiti. Kwa hivyo hilo halidhuru kitu na wala haliathiri swalah za waswaliji. Lakini upande wa Qiblah cha msikiti kukiwa na kitu basi salama zaidi kuwepo kati ya msikiti na makaburi ukuta mwingine mbali na ule ukuta wa msikiti au kuwepo na njia inayopambanua kati ya viwili hivyo. Hili ndio salama na bora zaidi ili hilo liwe mbali zaidi na kuyaelekea makaburi.

Lakini yakiwa upande wa kulia au upande wa kushoto kwa wenye kuswali haidhuru kitu kwa sababu hawayaelekei. Kwa sababu hili liko mbali zaidi na kuyaelekea na utata wa kuyaelekea.

Kuhusu kuegesha magari ni jambo lisilofaa kuyaegesha juu ya magari. Yaegeshwe mbali na makaburi katika ardhi salama zisizokuwa na makaburi. Kwa sababu haijuzu kwa watu kuyatwezwa makaburi au kuyaweka magari kwenye makaburi. Haya ni maovu na haijuzu. Ni lazima kuyaweka mbali na makaburi na kuyaweka maeneo salama ambapo hakuna makaburi. Ikiwa ni wepesi kuyawekea uzio kwa njia itakayozuia kuyakanyaga na kuyadhalilisha basi ndio salama na salama zaidi. Kwa sababu muislamu ni mwenye kuheshimiwa akiwa hai na baada ya kufa. Kwa ajili hii ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akakataza kuswali kuyaelekea makaburi na kukaa juu yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr min Fitnat-il-Qubuur, uk. 76-77
  • Imechapishwa: 05/05/2022