2- Halafu kunafuata majina yote ya Allaah mazuri ambayo mtu anajithibitishia uja. Mfano wa majina hayo ni “´Abdul-´Aziyz”, mja wa Mwenye nguvu kabisa, na “´Abdul-Malik”, mja wa Mfalme. Watu wa kwanza kuitwa hivo ni wavulana wawili wa Marwan bin al-Hakam.

Raafidhwah hawana majina haya mawili kwa sababu ya kuonyesha kujitenga kwao mbali na Banuu Umayyah. Si jengine isipokuwa uadui na chuki. Huo ndio msimamo wao juu ya majina mengine waliokuwa nayo watu katika Banuu Umayyah kama vile Mu´aawiyah, Yaziyd, Marwaan, Hishaam… Kadhalika wamejiharamishia jina la “´Abdur-Rahmaan” kwa sababu aliyemuua ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa anaitwa ´Abdur-Rahmaan bin Muljam.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 18/03/2017