18. Maimamu wanne wana ´Aqiydah moja

… na kitu katika adabu zake na jumla katika misingi na fani za Fiqh kwa mujibu wa madhehebu na njia ya Imaam Maalik bin Anas (Rahimahu Allaah) – Misingi ya Fiqh ni zile kanuni zake zilizonyofolewa kutoka katika dalili na ubainifu wa hukumu ambazo ni halali, haramu, mambo ya wajibu, mambo yaliyopendekezwa, mambo yaliyochukizwa na mambo yaliyoruhusiwa.

Kuhusu kanuni zilizonyofolewa kutoka katika dalili, ni masuala yanayohusiana na kwamba amri inapelekea katika ulazima au katika mapendekezo au kuruhusiwa na kama makatazo yanapelekea katika uharamu au machukizo.

Maalik bin Anas alikuwa ni mwanachuoni wa al-Madiynah. Alikuwa ni imamu wa mji wa uhamiaji. Madhehebu yake ni moja katika yale madhehebu manne. Mtunzi wa kitabu alikuwa mwenye kufuata madhehebu ya Maalik katika Fiqh. Ndio maana akatunga kitabu hiki kutokana na madhehebu ya Maalikiyyah. Hata hivyo ´Aqiydah ya maimamu wanne ilikuwa moja; ´Aqiydah ya Salaf. Hawakuwa ni wenye kutofautiana kati yao katika jambo hilo.

Madhehebu ya Imaam Maalik yalienea Magharibi, Andalusia na Afrika. Madhehebu yale yalikuwa ndio madhehebu ambayo yanatendewa kazi na wanachuoni al-Madiynah. Lakini Hata hivyo ´Aqiydah hii haikufupika kwa Imaam Maalik (Rahimahu Allaaah) peke yake. Lakini kwa vile watu wa Magharibi, akiwemo mtunzi wa kitabu, wanamfuata Maalik, ndio maana ikawa ni jambo munasibu kubainisha ´Aqiydah na mengineyo kwa mujibu wa madhehebu yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 21-22
  • Imechapishwa: 08/07/2021