Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Hilo Allaah amewaamrisha watu wote na amewaumba kwa lengo hilo. Allaah (Ta´ala) amesema:

 وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ

“Sikuumba majini na watu isipokuwa waniabudu.” (adh-Dhaariyaat 51 : 56)

MAELEZO

Hilo… – Bi maana kwa Hanafiyyah ambayo maana yake ni kumwabudu Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini. Allaah amewaamrisha watu wote na akawaumba kwa lengo hilo. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ

“Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana mungu wa haki isipokuwa Mimi – hivyo basi Niabuduni.” (al-Anbiyaa´ 21 : 25)

Allaah (´Azza wa Jall) amebainisha katika Kitabu Chake kwamba viumbe wameumbwa kwa lengo hili tu. Amesema (Ta´ala):

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ

“Sikuumba majini na watu isipokuwa waniabudu.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 38-39
  • Imechapishwa: 19/05/2020