Msafara wa kwanza wa kijeshi ambao Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamrisha ilikuwa ni msafara wa Abwaa´. Ulikuwa katika Safar miaka miwili baada ya kuhajiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwenyewe alishiriki katika msafara huo wa kijeshi. Alipofika Waddaan akafunga amani na Banuu Dhamrah bin Bakr bin ´Abdi Manaah bin Kanaanah na mkuu wao wa kabila Makhshiy bin ´Amr. Kisha akarudi al-Madiynah pasi na vita. Katika kipindi hicho alikuwa amemuacha Sa´d bin ´Ubaadah (Radhiya Allaahu ´anh) kuwa khalifa al-Madiynah.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 41
  • Imechapishwa: 25/04/2018