18. Inajuzu kuacha Tawhiyd na badala yake kulingania katika ukhaliyfah?


Swali 18: Ni yapi maoni yako kwa mwenye kusema kwamba inatakikana kwetu hii leo kutumia juhudi zetu kusimamisha ukhaliyfah mwongofu. Je, maelezo haya ni sahihi au ni makosa?

Jibu: Maelekezo haya ni makosa mia kwa mia. Allaah (Subhaanah) amesema kuwaambia Mitume Wake (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam):

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

Hakika Tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na miungu ya uongo.”[1]

Aliwaamrisha walinganie katika Tawhiyd. Kadhalika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum), wafuasi wake wote, katika kila wakati na mahala, wanalingania katika Tawhiyd na katika msingi ambao dini hii imesimama juu yake. Pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomtuma Mu´aadh kwenda Yemen alimwambia:

“Walinganie watu katika kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Wakikutii katika hilo, waeleze kuwa Allaah amefaradhisha juu yao swalah tano asubuhi na jioni… “

Kwa hivyo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameamrisha kulinganiwe katika Tawhiyd na katika msingi wa dini. Kadhalika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kulinganiwe katika Tawhiyd na katika msingi wa dini.

Tukisema kwamba tulingania katika ukhaliyfah basi tutakuwa tumeacha msingi ambao tumeamrishwa na Allaah na Mtume Wake na tutakuwa tumeleta msingi mwingine. Kuhusu ukhaliyfah uliisha tangu zamani pale ambapo Allaah atataka. Hatujawabishiwa kulingania katika ukhaliyfah. Allaah ametuwajibishia kulingania katika Tawhiyd. Ambaye atalingania katika ukhaliyfah basi ameacha jambo ambalo Allaah amemuwajibishia na badala yake ameleta jambo ambalo amelazimishwa na watu wa pote lake. Allaah (Ta´ala) amesema:

أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ

“Je, wanao washirika waliowaamuru dini yale ambayo Allaah hakuyatolea idhini?”[2]

Ukhaliyfah Allaah ndiye ataupanga pale ambapo atajitokeza yule mtu kutoka katika familia ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Naye si mwengine ni Mahdiy. Huu ndio ukhaliyfah utaokuwepo pale ambapo Allaah atataka  na sio wakati sisi tutataka.

Kitendo cha wao kufanya bidii kuuleta ni jambo la batili na nia hii kadhalika ni batili. Haijuzu kwao kuacha kulingania katika dini ya Allaah kwa sababu ya jambo hilo. Madai yao haya malengo ni siasa na kutaka kufikia viti vya uongozi.

[1] 16:44

[2] 42:21

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 16/07/2017