18. Huyu pekee ndiye kamfahamu al-Albaaniy

Nchi yetu inatambulika vyema namna inavyotangamana na watu ambao sio wazuri ipasavyo. Tusemeje juu ya mwanachuoni miongoni mwa wanachuoni wa waislamu ambaye ana ´Aqiydah ya Salafiyyah, mwenye kuifuata Sunnah na ambaye ameitumikia Sunnah kwa kiasi kikubwa? Nchi kama hii yetu haitakiwi kuwasikiliza watu wabaya na watu waliojawa na matamanio ambao Allaah pekee ndiye anayejua malengo yao.

Kwa hayo imepata kubainika kwamba utumiaji wa Shaykh (Rahimahu Allaah) neno “kupambana” hakusudii kupambana kwa silaha, bali anachokusudia ni upambanaji wa mafunzo na kulingania katika Qur-aan na Sunnah kwa ufahamu wa Salaf. Aliutumia umri wake mrefu uliobarikiwa katika uandishi wake, nasaha na mijadala. Yule atakayesoma vitabu vyake na wasifu wake, basi atabainikiwa na hayo waziwazi. Ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba njama za wenye mashaka dhidi yake ni uongo wa wazi na uzushi ambao Allaah pekee ndiye anajua malengo yao.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 41
  • Imechapishwa: 30/11/2018